Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Tuesday, March 5, 2013

NAIBU WAZIRI WA UJENZI Eng.Gerson Lwenge LEO AMEENDELEA NA ZIARA YAKE JIMBONI KWAKE.


Mbunge Lwenge akiwa kwenye uwanja wa mkutano katika kijiji cha Mawindi kata ya Igima Wilayani Wanging'ombe.
Wananchi wa kijiji cha Mawindi wakimsikiliza mbunge wao leo kijijini humo.
Mbunge Lwenge akiwakabidhi vijana mpira wa miguu katika harakati za kupunguza maambukizi ya Gonjwa la Ukimwi kimichezo.
Mbunge Lwenge akizungumza na mkazi wa kijiji cha Mawindi leo.

Wananchi wa kijiji cha Mawindi wakitawanyika mara baada ya kuahirishwa kwa mkutano huo

Hapa wananchi wakiondoka baada ya kuhitimishwa kwa mkutano wa Mbunge Lwenge kijijini humo leo.

Safari ya Naibu Waziri wa Ujenzi Eng.Gerson Lwenge ikiwa imeiva ya kurudi kijijini kwake Dulamu mara baada ya Kuhitimisha mkutano wa hadhara kijijini Mawindi leo.

Naibu waziri wa ujenzi Mhandisi Gerson Lwenge ambaye ni mbunge wa Jimbo la Njombe Magharibi leo Ameendelea na ziara yake ya kuwatembelea wananchi wake na kukagua shughuli za maendeleo ikiwa ni pamoja na kuchochea shughuli hizo.
Ziara hiyo imeanza tangu machi Mbili mwaka huu kwa kuzungukia  vijiji vya Ikwavila ambako alichangia kiasi cha shilingi laki saba kwa ajili ya ukarabati wa shule, katika kijiji cha  Ukomola alichangia kiasi cha shilingi milioni moja kufuatia madiwani kufanya harambee ya ujenzi wa shule ya msingi Ukomola wakati wa maadhimisho ya miaka 36 ya kuzaliwa kwa ccm  yaliyofanyika kijijini humo.

Aidha pia machi tatu mwaka huu mbunge huyo ametembelea mradi wa maji wa Mbukwa katika vyanzo vyake vya Masaulwa na kuwahakikishia wakazi wa kijiji hicho kuanza kutumia maji bomba mara baada ya kuzinduliwa kwa mradi huo.

Katika hatua nyingine siku ya jana mbunge Lwenge ametembelea kijiji kipya cha Mawindi chenye zaidi ya wakazi wapatao mia sita na hatimaye kuzungumza na wakazi hao.

Bisagi Mbanga ni Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Mawindi ambaye amesoma taarifa ya kijiji hicho na kubainisha changamoto mbalimbalimbali ikiwemo ya uchakavu wa shule ya msingi Mawindi.

Kufuatia taarifa na changamoto hizo mbunge Lwenge akasimama na kuchangia kiasi cha shilingi milioni moja ili zisaidie ukarabati wa shule hiyo huku akiwahimiza kuongeza jitihada katika shughuli za kimaendeleo.

Mapema kesho mbunge huyo atafanya ziara katika kijiji cha Itambo kilichopo kata ya Mdandu ambako utafanyika uwekaji saini ya mkataba wa ujenzi wa zahanati na nyumba ya mganga na ubalozi wa Japan na kisha machi sita mwaka huu atahitimisha ziara yake katika vijiji viwili vya kata ya Imalinyi kikiwemo kijiji cha Kinenulo.

No comments:

Post a Comment