Saturday, March 2, 2013
MTU MMOJA AMETUMBUKIA KWENYE BWAWA LA MAJI KATIKA MSITU WA KAMPUNI YA TANWAT MJINI NJOMBE,MAMIWA YA WATU WA NJOMBE WAKUSANYIKA KUTAFUTA MWILI WA MAREHEMU LEO.
Hili ndilo bwawa alilotumbukiwa Mexon Nyekelela Chota mkazi wa kibena kata ya Ramadhani mjini Njombe.
Hadi muda huu mwili wa marehemu haujaweza kufanikiwa kuonekana bado jitihada zinaendelea.
Wengine kwa mitumbwi wengine kwa madumu zote hizo ni jitihada za kuupata mwili wa marehemu.
Huyu ni kiongozi wa kampuni ya Tanwat meneja mwajiri na Utawala bwana Elly Sevele akionesha ushirikiano wa kuutafuta mwili wa marehemu.
Kabla marehemu hajatumbukia kwenye bwawa hili la maji walisimama kwenye kibanda hiki ili kujikinga na mvua baada ya hapo wakaingia kuogelea ndiyo kuzama baada ya kukosa pumzi.
Jitihada za wananchi bado zinaendelea kuutafuta mwili wa marehemu na hii ni nyavu walioiweka ili kuupata mwili wake lakini wamepata masalia ya mitumbwi iliyo tumbukia zamani na hapa wanaweka vizuri waendelee na utafutaji.Ni Tanwat kibena.
Mkazi Mmoja wa Kibena Mjini Njombe Mexon Nyekelela Chota Anadaiwa Kufariki Dunia Baada ya Kuzama Kwa Siku ya Pili Katika Mabwawa ya Kampuni ya TANWAT Mjini Njombe.
Kwa Mujibu wa Mashuhuda wa Tukio Hilo Wamesema Kuwa Mtu Huyo Alizama Jana Majira ya Saa Kumi na Moja Jioni Wakati Wakiendelea na Shughuli Zao za Sanaa na Ndipo Akazama Katika Mazingira ya Kutatanisha.
Akielezea Tukio Hilo Katibu wa Kikundi cha Sanaa Cha Kibena Arts Group Renato Mbuya maarufu kwa jina la Cash P Ameelezea Namna Tukio Hilo Lilivyotokea.
Pasval Kaduma ni Mwenyekiti wa Mtaa wa Kibena Hospitali Amethibitisha Kutokea Kwa Tukio Hilo na Kuwaomba Wananchi Kuendelea Kushirikiana Wakati Serikali Ikijipanga Kutafuta Vifaa na Wataalam wa Uzamiaji Huku Meneja Mwajiri na Utawala wa Kampuni ya Tanwatt Bwana Elly Sevele Akiahidi Kuongeza Ulinzi Katika Bwawa Hilo.
Mpaka kundi zima la wananchi na viongozi wa serikali za vijiji na kampuni wanaondoka eneo la tukio majira ya saa moja jioni maiti ilikuwa haija patikana na zoezi hilo wameazimia kuendelea tena kesho jumapili.
Kwa mujibu wa maelezo ya wazawa wa mtaa huo akiwemo mwenyekiti wa mtaa wa kibena kati Mwenda imedaiwa Katika eneo hilo kihistaria miaka ya 1970 mpaka 1973 kuna wahindi wawili waliwahi kutumbukia kwenye bwawa hilo na kupoteza maisha ambapo walipatikana baada ya siku saba wakiwa wamekufa maji na kuliwa na samaki kwa baadhi ya sehemu za miili yao.
Endelea kusoma taarifa hii kwa taarifa kamili tutakujuza endelea kupitia mtandao huu.Picha na Michael Ngilangwa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
ASANTE KWA JUHUDI ZENU KWA TAARIFA HADI SASA MCHANA HUU MWILI WA MAREHEMU UMEFANIKIWA KUKUTWA UKIELEA JUU YA MAJI.BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA. JNA LA BWANA LIBARIKIWE.
ReplyDeleteNGAILO JAMES- MOSHI UNIVERSITY-SHINYANGA