.....................................................................................................................................................................
WAKATI mtuhumiwa wa
mauwaji ya aliyekuwa mwandishi wa
kituo cha runinga cha Chanel Ten mkoani Iringa
Daudi Mwangosi askari wa FFU mwenye namba G2573 Pasificus
Cleophace Simoni (23) akitarajiwa kufikishwa tena mahakamani leo kwa kesi hiyo kutajwa ,askari wilaya ya Makete mkoa wa Njombe wadaiwa
kufanya mauwaji ya kinyama kwa
kumpiga mteja wa benki ya NMB kwa risasi .
Huku askari askari
mmoja nayetuhumiwa kufanya
unyama huo aliyetambulika
kwa jina moja la Jose akishikiliwa
na jeshi
la polisi kufuatia mauwaji hayo
ya kinyama.
Tukio hilo limekuja
huku bado watanzania hasa
wakazi wa mikoa
ya Iringa na Njombe wakiwa bado hawajasahau mauwaji ya
kinyama yaliyomkuta mwanahabari Daudi Mwangosi ambapo kesi hiyo bado ikiendelea kutajwa na wanahabari waliokuwepo eneo la tukio siku ya mauwaji wakisubiri
kuchukuliwa maelezo yao kama mashahidi
wa kesi hiyo pindi itakapoanzwa
kusikilizwa.
Mwandishi wa
mtandao huu kutoka
Makete Njombe anaeleza kuwa tukio
hilo wamedai kuwa mauwaji hayo ya kinyama
yametokea jana jumatano majira ya
saa 1.20 usiku baada ya mteja huyo
aliyekuwa na usafiri wa
boda boda kufika
eneo hilo la benki kwa lengo la kuchukua
fedha .
Imedaiwa kuwa aliyepigwa
risasi anatambuliwa kwa jina la Casto Kawambwa
mkazi Mbalizi mkoani Mbeya na kuwa
baada ya kupigwa risasi alikimbizwa katika
Hospitali ya wilaya ya
Makete ambako inadaiwa kabla ya kupatiwa matibabu amefariki dunia
.
Kutokana na tukio hilo
jeshi la polisi liliwazuia
wanahabari kutimiza wajibu
wao kwa kupiga picha
wala kusogea eneo hilo la Hospitali na badala yake kuweka
ulinzi mkali eneo hilo la Hospitali ili
kuzuia wanahabari kusogea
eneo hilo .
Hata hivyo
mmoja kati ya askari ambae jina lake halikufahamika mara moja alisikika akidai kuwa
chanzo cha mteja huyo wa benki kupigwa
risasi alikuwa akihisiwa kuwa ni jambazi na hivyo
baada ya kufika eneo hilo
kwa usafiri wake wa piki
piki (boda boda ) walihisi kuwa amefika kwa ajili ya
kufanya vitendo vya uporaji
katika benki hiyo na hivyo
askari katika hali ya kujihamia
aliamua kumpiga risasi .
Jitihada za
kumtafuta kamanda wa
polisi wa mkoa
wa Njombe ili kuzungumzia
undani wa tukio
hilo linafanyika na mtandao huu .
No comments:
Post a Comment