Mkuu wa Wilaya ya Wanging'ombe Esterina Kilasi akiwasili katika uwanja wa sherehe kata ya Uhambule hapo jana.
Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Fulgence Ngonyani akiwasili nae eneo la sherehe za wanawake.
Mkuu wa mkoa wa Njombe Captain Mstaafu Aseri Msangi baada ya kutelemka kwenye gari lake anaangalia Ngoma mbalimbali zikitumbwiza.
Ngoma ya asili limudoya ikichezwa siku ya wanawake duniani .
Hii ni safu ya sekretariet ya mkoa wa Njombe ikiongozwa na mkuu wa mkoa wa Njombe Captain Mstaafu Aseri Msangi.
NJOCOBA WAKIWA KATIKA MAONESHO SIKU YA WANAWAKE DUNIANI WILAYA YA WANGING'OMBE ILIYOFANYIKIA KATA YA UHAMBULE.
AKINA MAMA WAKIFURAHI NA KUCHEZA NGOMA UHAMBULE.
B . ALON AKIWA STEJINI AKIFANYA MAONESHO KWA KUIMBA MUZIKI WA KIZAZI KIPYA WA BONGO FRAVER NA WIMBO WAKE UNAOMTAMBULISHA NCHINI TANZANIA NA AFRIKA MASHARIKI KWA UJUMLA WA KOMBOLELA HAPA YUPO NA WENZAKE, NI SIKU YA WANAWAKE DUNIANI HAPA NI UHAMBULE.
KWAYA NAZO HAZIKUBAKI MBALI ZA KATA YA UHAMBULE .
KABLA MKUU WA MKOA HAJAENDA KUKAGUA MABANDA YA WAJASILIAMALI.
MKUU WA MKOA WA NJOMBE MSANGIN AKITEMBELEA KUFANYA UKAGUZI WA MABANDA YA MAONESHO MBALIMBALI YA WAJASILIAMALI WAFUGAJI NA MIRADI MINGINE.
KATIBU WA MUJATA AKIHOJIWA NA MKUU WA MKOA WANAFANYAJE KAZI ZAO NA JAMII INANUFAIKAJE NA MUJATA.
AFISA MAENDELEO WA HALMASHAURI YA WILAYA YA NJOMBE ABRAHAM KAAYA AKITOA TAARIFA FUPI MBELE YA MGENI RASMI.
HOTUBA YAKE MKUU WA MKOA WA NJOMBE CAPTAIN MSTAAFU ASERI MSANGI KWA WANANCHI.
WALIOSIMAMA NI KAMATI YA ULINZI NA USALAAMA MKOA WA NJOMBE IKIONGOZWA NA KAMANDA WA POLISI MKOA WA NJOMBE ACP FULGENZI NGONYANI WAKIJITAMBULISHA.
Ndivyo ilivyokuwa jana katika maadhimisho ya siku ya Wanawake Katika wilaya ya Wanging'ombe mkoani Njombe.
MKUU WA CHUO CHA MAENDELEO YA JAMII ULEMBWE MWALIMU FRANCIS HAULE,
Akiwa na wanachuo ambao walikatishwa masomo kwa kupata ujauzito wakiwa shuleni na hapa wamepata elimu ya ufundi stadi inayowasaidia kujikwamua na maisha na familia zao baada ya kutengwa na wazazi wao.Picha na Michael Ngilangwa.
SIKU YA WANAWAKE DUNIANI.
Akizungumza na wananchi wa kata ya Uhambule katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani Captain Msangi amesema wanawake wanatakiwa kujishughulisha katika shughuli za miradi ya maendeleo ikiwemo kuwania fursa mbalimbali za uongozi serikalini ili kuweka haki sawa na wanaume huku akikemea matendo unyanyasaji kwa watoto wadogo matendo yanayofanywa na baadhi ya wanawake na wanaume.
Aidha mkuu wa mkoa wa Njombe Msangi amesema wanawake wanatakiwa kufahamu maana ya masuala ya jinsia ndipo matendo ya unyanyasaji wa kijinsia yaweze kupigwa vita mahala popote mkoani Njombe na kusema kuwa kila mwaka wanawake huadhimisha sherehe hiyo ili kuhamasisha uwepo wa uhuru na kupigania haki,kupinga ukatili wa kijinsia katika maisha ya jamii ya kila siku.
Hahata hivyo Amesema kufuatia matendo yanaendelea ya kutumikishwa kazi ngumu kwa akina mama waliowengi wa maeneo ya vijijini ni dhahiri kuwa bado miongoni mwa jamii hakujawa na usawa kutokana na wanaume kuwaachia baadhi ya kazi wanawake huku wakitakiwa kushirikiana kwa pamoja kufanya kazi zote pasipo ubaguzi ikiwemo umiliki wa mali za urithi kwa wanawake.
Pamoja na kuhimiza uwepo wa uwiano katika familia na jamii yote Captain Msangi pia amehamasisha wanawake kujikita katika miradi mbalimbali ya kimaeendeleo ikiwemo kushiriki katika kilimo cha mazao ya alizeti,mahindi,karanga na mazao mengine kwa kutumia mbolea ili kupata mazao ya kutosha yatamsaidia mwanamke kujikwamua kiuchumi.
Pia ametoa agizo kwa maafisa taraafa na maendeleo mkoani Njombe kujitahidi kuongeza Bengi za wakulima wa vijijini VICOBA ambavyo vitawasaidia kuweka akiba na kupata mikopo ili kunufaika na mikopo hiyo huku akisisitiza wazazi kuwapeleka watoto shuleni na kinyume na hapo afisa mtendaji wa kata ya Uhambule awafikishe mahakamani watakao kaidi agizo hilo kuanzia march 20 mwaka huu.
Afisa maendeleo wa halmashauri ya Wilaya ya Njombe bwana Abraham Kaaya amesema matendo ya unyanyasaji wa kijinsia wilayani Njombe umekithili kutokana na kuripotiwa kwa matukio ya kudhalilishwa kwa watoto ambao hupigwa na kufungwa kamba na wazazi wao,wanawake hupigwa na waume zao,wazee kuuwawa kwa imani za kishirikina na kusema kuwa kutokana na hali hiyo ya kunyanyaswa kwa watoto na akina mama imepelekea ongeeko la watoto wa mitaani.
Aidha bwana Kaaya amesema uzoefu unaonesha kuwa wanawake wengi hawamiliki mali zenye thamani na kusema kuwa wengi wao humiliki mali ndogondogo ikiwemo samani,vyombo vya jikoni, mazao ya viazi ambapo mashamba hupewa kwaajili ya kutumia tu na mali kubwa humikiwa na wanaume hali inayopelekea wanawake kushindwa kutoa maamuzi katika mali hizo.
No comments:
Post a Comment