Sunday, February 10, 2013
VIONGOZI WA CHAMA CHA MAPINDUZI WATEMBELEA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO KATA YA NJOMBE MJINI.
Viongozi wa chama cha mapinduzi kata ya Njombe mjini wakipanda miti siku ya maadhimisho ya kutimizaq miaka 36 ya kuzaliwa kwa chama hicho.
Diwani viti maalumu Kata ya Njombe mjini alitembelea shule ya Joseph Mbeyela.
Msingi wa choo kipya katika shule ya sekondari Joseph Mbeyela.
Chama cha Mapinduzi Kata ya Njombe Mjini Kimefanya Maadhimisho ya Miaka 36 ya Kuzaliwa Kwa Chama Hicho Ambapo Pamoja na Mambo Mengine Wanachama na Viongozi wa CCM wa Kata Hiyo na Tawi Wakiongozwa na Mwenyekiti wa UWT Kata ya Njombe Mjini Bi. Angela Mwangeni Wametembelea na Kukagua Miradi Mbalimbali ya MAendeleo Inayotekelezwa Katika Kata Hiyo.
Akiongea Kwenye Maadhimisho Hayo Bi. Mwangeni Ambaye Alikuwa Mgeni Rasmi Amewataka Wakazi wa Mitaa ya Njombe Mjini Kushirikiana Kwa Pamoja Ili Kufanikisha Shughuli za Miradi ya Maendeleo Ndani ya Kata Yao Hali Ambayo Itasaidia Kusogeza Huduma za Kijamii Karibu na Wananchi.
Akisoma Taarifa ya Mtaa wa Mgendela Mbele ya Mgeni Rasmi Afisa Mtendaji wa Mtaa Huo Bwana Mashaka Lulambo Ameelezea Juu ya Ujenzi wa Ofisi ya Mtaa wa Mgendela Ambayo Itagharimi Kiasi cha Shilingi Milioni 30 Hadi Kukamilika Kwake Ambapo Hadi Hivi Sasa Zaidi ya Shilingi Milioni Tano Zimetumika Katika Ujenzi Huo, na Pia ameelezea Baadhi ya Changamoto wanazokutana Nazo Katika Utekelezaji wa Majukumu Yao.
Naye Mwenyekiti wa Mtaa Huo Bwana Kasimu Mlula Ameiomba Serikali Kuwasaidia Wananchi wa Mtaa Huo Kulitafutia Ufumbuzi Tatizo la Maji Linalowakabili Wakazi wa Mtaa Huo , Huku Akikemea Baadhi ya Wakazi wa Mtaa Huo Wanaoendesha Shughuli za Kiuchumi na Kujenga Kwenye Vyanzo Vya Maji
Katika maadhimisho hayo viongozi wa chama cha mapinduzi kata ya Njombe mjini walitembelea miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa shule mpya ya msingi Ruhuji,shule ya msingi inayojengwa mtaa wa Idundilanga,zahanati ya Idundilanga na kugawa zawadi kwa wagonjwa za sabuni na mafuta pamoja na kukagua ujenzi wa ofisi ya mtaa wa Mgendela.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment