Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
CHAMA
Cha Mapinduzi(CCM) kupitia viongozi wake wa ngazi mbalimbali
wameendelea kunadi sera za maendeleo na kumuombea kura mgombea wao wa
ubunge kwenye uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kinondoni jijini Dar es Salaam
huku baadhi yao wakisema uchaguzi huo ni sawa na usajili wa dirisha
dogo.
Hivyo
wanatumia usajili huo kwa ajili ya kumpata Mtulia ambaye wanaamini ni
mtu sahihi kwa maendeleo ya wananchi wa Kinondoni kwani alikokuwa awali
hakuwa nafasi ya kushirikiana na Serikali ya Rais ,Dk.John Magufuli
kufanya maendeleo.
Wakizungumza
kwenye kampeni za uchaguzi huo unaotarajia kufanyika Februari
17(Jumamosi ya wiki hii), viongozi wa CCM wakiwamo baadhi ya mawaziri
ambao wamefika kwenye kampeni hizo kwa nafasi zao za ubunge,wamewaambia
wananchi hao Mtulia ndio mtu sahihi kwao.
Mgeni
rasmi kwenye kampeni zilizofanyika leo Kata ya Ndugumbi ambaye pia ni
mbunge wa Mbinga Sixtus Mapunda amesema anatambua uwezo wa Mtulia na
hivyo ni vema wananchi wakamchagua ili awatumikie kikamilifu.
Amewaeleza
wananchi kuwa uchaguzi mkuu ulishafanyika mwaka 2015 na sasa ni
uchaguzi mdogo ,hivyo Chama ambacho kimepewa dhamana ya kuongoza ni CCM
na kwa maana hiyo Mtulia akiwa mbunge atashirikiana na viongozi wengine
kuleta maendeleo ya wananchi.
Amefafanua
anaufananisha uchaguzi huo na usajili wa dirisha dogo ambapo tayari CCM
wanayo timu nzuri yenye ushindani wa hali ya juu na iliyokuwa na ari ya
kuwatumikia wananchi,hivyo kwenye usajili huo wanamtaka Mtulia
kuboresha timu yao.
"CCM
ni timu ambayo inawachezaji wazuri na waliotumia kwenye kila idara na
kama mnavyojua kwenye usajili mdogo lazima msajili mchezaji ambaye
atakuwa na uwezo na anaendana na kasi na timu ambayo tunayo.Hivyo Mtulia
ni mtu sahihi kwetu.
"Kule
alikokuwa mwanzoni hakuwa na uwezo wa kufanya maendeleo kwani kila
akitaka kufanya wenzake wanamzuia kwa kigezo kuwa yakipatikana maendeleo
ya Kinondoni upinzani hautakuwa na nafasi mwaka 2020.Hivyi akiwa CCM
atafanya maendeleo kwa kasi kubwa na tutampa ushirikiano kadri ya uwezo
wetu,"amesema Mapunda.
No comments:
Post a Comment