Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa,
akimsikiliza kwa makini Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri (kushoto),
alipomtembelea ofisini kwake katika ziara yake ya kikazi mkoani humo
kwa lengo la kukagua miradi ya ujenzi ya barabara iliyokamilika na
inayoendelea. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Tabora, Queen Mlozi.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akizungumza
na uongozi wa Wilaya ya Urambo, alipokutana nao katika ziara yake ya
kikazi ya kukagua mradi wa ujenzi wa barabara ya Urambo-Kaliua yenye
urefu wa KM 28 inayojengwa kwa kiwango cha lami, mkoani Tabora.
Mbunge
wa jimbo la Urambo, Mhe. Magreth Sitta, akimshukuru Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kulia), kwa kufuatilia
maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Urambo-Kaliua yenye urefu wa KM 28
inayojengwa kwa kiwago cha lami, mkoani Tabora.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akizungumza
na waandishi wa habari (hawapo pichani), kuhusu hatua za mradi wa
ujenzi wa barabara ya Urambo-Kaliua yenye urefu wa KM 28 na kusisitiza
nia ya Serikali ya kuwajengea uwezo wakandarasi wazawa ili waweze
kutekeleza miradi ya ujenzi hapa nchini.
Mbunge
wa jimbo la Urambo, Mhe. Magreth Sitta, akiagana na Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, mara baada ya kukagua
ujenzi wa barabara ya Urambo-Kaliua yenye urefu wa KM 28 kwa kiwango cha
lami, mkoani Tabora.
Muonekano
wa Daraja la Kasisi lenye urefu wa mita 54 lililopo katika barabara ya
Tabora-Pangale yenye urefu wa KM 30. Ujenzi wa barabara hiyo umefikiwa
asilimia 80 na inajengwa na mkandarasi CICO kwa gharama ya shilingi
bilioni 28.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, Mkuu wa
Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri, na uongozi wa wilaya ya Tabora wakipita
juu ya daraja la Wala lenye urefu wa mita 34 katika barabara ya
Tabora-Pangale yenye urefu wa KM 30, katika ukaguzi wa ujenzi wa
barabara hiyo, mkoani humo.
…………………
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, amewataka
makandarasi wazawa wa kampuni ya Samota, Anam na Jossam JV wanaojenga
barabara ya Urambo-Kaliua yenye urefu wa KM 28 kwa kiwango cha lami
wahakikishe wanakamilisha ujenzi wa barabara hiyo kwa muda uliowekwa.
Prof.
Mbarawa ametoa agizo hilo katika kijiji cha Motomoto, Wilaya ya Urambo
mkoani Tabora alipokuwa katika ziara yake ya kikazi ya kukagua mtandao
wa barabara mkoani humo na kutoridhishwa na kasi ya ujenzi wa barabara
hiyo.
“Nataka
nione kazi za ujenzi zinafanyika kwa haraka, kwani uzoefu unaonesha
baadhi ya makandarasi wazawa wamekuwa na kasi ndogo, hivyo mjipange
vizuri ili barabara ikamilike kwa wakati”, amesema Prof. Mbarawa.
Amesema
kuwa nia ya Serikali ni kuwajengea makandarasi wazawa uwezo ili waweze
kutekeleza miradi mikubwa mingine ya ujenzi hapa nchini lakini haitasita
kuwanyima kazi hizo kama miradi hiyo itacheleweshwa, haitakidhi viwango
vinavyohitajika na kama hawataonekana eneo la kazi kwa kipindi kirefu.
“Mkandarasi
mzawa atakayechelewesha mradi wowote wa ujenzi hatapewa kazi nyingine
kwa sababu atakuwa amechelewesha maendeleo ya wananchi”, amesisitiza
Prof. Mbarawa.
Ameongeza kuwa Serikali imejipanga kuwalipa makandarasi wazawa kwa wakati ili waweze kutekeleza miradi yao kwa ufanisi.
Naye
Mbunge wa jimbo la Urambo, Magreth Sitta, amemueleza Waziri Prof.
Mbarawa kuwa ujenzi wa barabara hiyo ni muhimu kwa wananchi wa wilaya
yake na Kaliua na hata mikoa jirani kwani usafirishaji wa mazao na
abiria utarahisishwa.
Kwa
upande wake Mkuu wa Wilaya ya Urambo, Angelina Kwingwa amesema
wamejipanga vyema kutoa ushirikiano kwa wakandarasi wazawa hao, na
kuahidi kumsimamia ili amalize kazi hiyo kwa wakati, lakini kwa kiwango.
Awali
akitoa maelezo ya mradi wa ujenzi wa barabara hiyo, Meneja wa Wakala wa
Barabara (TANROADS), mkoani humo Mhandisi Damian Ndibalinze, amesema
mkandarasi ameshapewa fedha za mradi hivyo hakuna sababu ya kuchelewesha
mradi huo na kuahidi kuwasimamia ili wakamilishe kabla ya mwaka 2020.
Ameongeza
kuwa ujenzi wa barabara hiyo utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 37.6
na zote zikiwa zinafadhiliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kwa asilimia 100.
Katika
hatua nyingine, Waziri Prof. Mbarawa amekagua ujenzi wa barabara ya
Tabora-Pangale yenye urefu wa KM 30 inayojegwa na mkandarasi CICO kwa
gharama ya shilingi bilioni 28.6 na kumtaka mkandarasi huyo kukamilisha
ujenzi wa barabara hiyo ifikapo mwishoni mwa mwezi wa sita.
Waziri
Prof. Mbarawa yuko mkoani Tabora kwa ziara ya siku mbili akiwa na lengo
la kukagua utekelezaji wa miundombinu ya barabara, mkoani humo
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
No comments:
Post a Comment