MKUU WA MKOA WA NJOMBE CHRISTOPHA OLE SENDEKA AKITOA MAAGIZO KWA HALMASHAURI YA MJI WA NJOMBE KUVUNJA MKATABA NA KAMPUNI YA IHAGALA AUCTION MART KUTOKANA NA KUINGIZWA KATIKA KAZI YA KUKUSANYA MAPATO BILA TARATIBU ZA MANUNUZI KUFUATWA, KUTANGAZA ZABUNI HAZIKUTANGAZWA NA UNYANYASAJI KWA WANANCHI NI MKUBWA UNAOFANYWA NA KAMPUNI HIYO.
VIONGOZI WA JUMUIYA YA WAFANYABIASHARA WA NJOMBE WAKIWA NA MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MJI WA NJOMBE PAMOJA NA MKUU WA WILAYA NA VIONGOZI WENGINE WA CCM KWENYE MKUTANO WA WAFANYABIASHARA NJOMBE MJINI.
WAFANYABIASHARA WAKIWA KWENYE UKUMBI WA TURBO KUTOA KERO ZAO DHIDI YA MSANGU.
MKURUGENZI WA KAMPUNI YA IHAGALA AUTION MART INAYOMILIKIWA NA CAROS MSANGU AKIJIBIA BAADHI YA HOJA ZINAZOMUHUSU YEYE NA KWANINI ANATUMIA GARI LA SERIKALI KWA KAZI ZAKE BINAFSI.
MWANASHERIA WA HALMASHAURI AKIWA NA MKURUGENZI WA IHAGALA AUCTION MART WAKISAIDIANA KUJIBU HOJA ZINAZOULIZWA NA WAFANYABIASHARA ZILIZOELEKEZWA KWA MKUU WA MKOA WA NJOMBE.
Mkuu Wa Mkoa Wa Njombe Christopha Ole Sendeka Ameagiza Kusimamishwa Kampuni Ya Ihagala Auction Mart Inayosimamiwa Na Caros Msangu Kutokana Na Kukiukwa Kwa Sheria Ya Manunuzi Na Kuagiza Kuvunjwa Kwa Mkataba Wake Na Halmashauri Ya Mji Wa Njombe .
Hatua Hiyo Ya Mkuu Wa Mkoa Wa Njombe Ole Sendeka Ya Kuisimamisha Kampuni Ya Ihagala Auction Mart Imetokana Na Malalamiko Ya Wafanyabiashara Kulalamikia Kampuni Hiyo Kutumia Mamlaka Vibaya Huku Wakisema Upatikanaji Wake Haukufuata Sheria Ya Kutangaza Zabuni.
Bwana Sendeka Amesema Kampuni Hiyo Imeonekana Kufanya Kazi Ya Kukusanya Mapato YHalmashauri Kwaajili Ya Viongozi Fulani ,Kutumia Gari La Serikali, Kuwakejeli Wafanyabiashara Ambapo Hata Alipotaka Kupewa Ufafanuzi Namna Ilivyopatikana Imeonesha Alikwenda Kiundugu.
Akijibu Maswali Ya Mkuu Wa Mkoa Wa Njombe ,Mkurugenzi Wa Kampuni Ya Ihagala Auction Mart Caros Msangu Amesema Yeye Anafanya Kazi Kwa Mujibu Wa Sheria Kwani Ana Mkataba Na Halmashauri Ya Mji Wa Njombe Wa Kukusanya Mapato .
Awali Wafanyabiashara Wamefikisha Kero Mbalimbali Kwa Mkuu Wa Mkoa Wa Njombe Christopha Ole Sendeka Kwamba Gari La Serikali Linatumiwa Na Kampuni Binafsi, Ukamataji Usiyo Na Staha, Uwepo Wa Tozo Zinazoashiria Kuomba Rushwa Huku Mwenyekiti Wa Jumuiya Ya Wafanyabiashara JWT Onesmo Mwajombe Akishukuru Kwa Maamuzi Hayo Ya Kuisimamisha Kampuni Hiyo.
Aidha Wafanyabiashara Hao Wamesema Kuwa Baadhi Ya Michango Hawana Imani Nayo Kwani Baadhi Ya Fedha Zinaishia Kwenye Mifuko Ya Kampuni Hiyo Ambayo Mkurugenzi Na Watalaamu Wa Halmashauri Ya Mji Wa Njombe Wameshindwa Kutolea Majibu Yakumuridhisha Mkuu Wa Mkoa.
Hivi Karibuni Kikao Cha Baraza La Madiwani Wa Halmashauri Ya Mji Wa Njombe Kiliwasimamisha Madiwani Watatu Akiwemo Diwani Wa Viti Maalumu Tarafa Ya Njombe Mjini Sekrada Mligo, Diwani Wa Kata Ya Ramadhani Geoge Sanga Na Diwani Wa Kata Ya Iwungiro Bwana Danda Ambao Walionekana Kushikilia Shilingi Ya Kutaka Ijadiliwe Hoja Ya Uwepo Wa Msangu Na Kusimamishwa Vikao Vitatu.
No comments:
Post a Comment