NAIBU WAZIRI KWANDIKWA AWATAKA TEMESA KUPELEKA KIVUKO LINDI
Mkuu
wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi akitoa taarifa kwa Naibu Waziri wa
Ujenzi, Elias Kwandika, kuhusu hali ya miundombinu ya barabara,
madaraja, vivuko, pamoja na viwanja vya ndege katika mkoa huo. Naibu
Waziri huyo yupo katika ziara ya kikazi ya siku 3 mkoani humo.
aibu
Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa akizungumza na uongozi wa mkoa wa
Lindi katika kikao kazi, kuhusu umuhimu wa wataalamu wote kushirikiana
katika masuala ya ujenzi wa miundombinu ya barabara katika mkoa huo.
Kulia ni Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Lindi,
Mhandisi Isaack Mwanawima akisikiliza.
Muonekano
wa ujenzi wa maegesho ya kivuko kitakachotoa huduma kati ya Lindi Mjini
na Kitunda, ambapo mkataba wa kukikokota Kivuko hiko kutoka Pangani
mkoani Tanga kuja Lindi upo katika hatua za mwisho.
Mbunge
wa Viti Maalum kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Lindi,,
Hamida Abdallah akimshukuru Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa
kufika mkoani hapo kwa ajili ya kutazama hali ya miundombinu ya
barabara, madaraja, vivuko na viwanja vya ndege.
Naibu
Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, na Mbunge wa Viti Maalum kwa tiketi
ya Chama cha Mapinduzi (CCM), mkoa wa Lindi, Mhe. Hamida Abdallah,
wakikagua ujenzi wa madarasa ya Shule ya Sekondari ya Lindi inayojegwa
na SUMA JKT chini ya uangalizi wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA),
katika ziara ya kikazi mkoani humo.
Naibu
Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, ameuagiza Uongozi wa Wakala wa
Ufundi na Umeme (TEMESA) makao makuu kusaini haraka mkataba kwa
mkandarasi atakayebeba kivuko kipya kutoka eneo kinapotengenezwa
wilayani Pangani mkoani Tanga hadi mkoani Lindi.
Akizungumza
mara baada ya kukagua maegesho ya kivuko hicho ambacho kinatarajiwa
kutoa huduma za usafiri kutoka Lindi Mjini - Kitunda mkoani humo, Naibu
Waziri huyo amewahakikishia wananchi kutegemea kupata huduma nzuri za
usafiri kwani ujenzi wa kivuko na maegesho yake kwa sasa umefika
katika hatua nzuri.
"Naagiza
Mamlaka husika kusaini haraka mkataba kwa mkandarasi atakayebeba kivuko
hiki kutoka Tanga hadi hapa ili wananchi waone kwamba kivuko kimefika
na kipo tayari kwa ajili ya kutoa huduma", amesema Naibu Waziri
Kwandikwa.
Aidha,
Naibu Waziri huyo ameridhishwa na ujenzi wa maegesho hayo ambayo kwa
sasa ujenzi wake umebakia asilimia 10 na hivyo kutarajiwa kukamilika
muda wowote.
Katika
hatua nyingine Naibu Waziri Kwandikwa, ametembelea na kukagua uwanja wa
ndege wa Lindi ambapo amesema Serikali inaendelea na mpango wake wa
kuboresha viwanja vya ndege nchini ili kuimarisha huduma katika usafiri
wa anga.
Amefafanua
kuwa Serikali kupitia mwaka wa fedha 2018/19 licha ya kuwa na mpango wa
kuboresha uwanja huo pia itaboresha Uwanja wa ndege wa Kilwa Masoko
lengo ni kuleta maendeleo kwa wananchi.
Kwa
upande wake Meneja wa TEMESA mkoani Lindi, Mhandisi Greyson Maleko,
amemhakikishia Naibu Waziri huyo kujipanga katika kuhakikisha wananchi
wa Lindi wanapata huduma bora za kivuko.
Naye,
Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), mkoani humo
Mheshimiwa Hamida Abdallah, ameipongeza na kuishukuru Serikali ya Awamu
ya Tano kwa kusogeza maendeleo kwa wananchi na kutatua changamoto
mbalimbali zinazowakabili.
Naibu
Waziri Kwandikwa amemaliza ziara ya kikazi ya siku Tatu mkoani humo
ambapo ametembelea na kukagua Miradi mbalimbali inayotekelezwa na Wizara
yake ili kujionea maendeleo na changamoto zake.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
No comments:
Post a Comment