UHARIBIFU
wa mazingira unaotokana na mabadiliko ya tabia nchi na shughuli za
kibinadamu kwenye bwawa la Mtera sio tu unaathiri kiasi cha maji kwa
matumizi ya Kituo cha kufua umeme cha Mtera bali pia unaathiri pakubwa
kituo kingine cha kufua umeme cha Kidatu mkoani Morogoro, Mtaalamu wa
Mazingira wa Shirika la Umeme nchini TANESCO, Bw. Yusuf Kamote
amewaambia waandishi wa habari waliotembelea Kituo cha Kufua Umeme wa
Maji cha Mtera, kilichoiko mpakani mwa mikoa ya Dodoma na Iringa.
Ukiachilia
mbali mabadiliko ya tabia nchi, shughuli za kibinadamu kandokando ya
mito, kunachafua mazingira ya mito hiyo na kupunguza kiasi cha maji na
hivyo kuathiri uzalishaji umeme wa maji.
“Tatizo hili ni kubwa
watu wanaingilia mito hii, kuna wakulima na wafugaji wanathiri sana,
shughuli za kilimo na ufugaji zinaleta mchanga mwingi kwenye maji na
hivyo kupunguza kina cha mto na maji yenyewe tunaita siltation, na hiyo
ikitokea ujio wa maji kwenye mitambo unapungua na hivyo uzalishaji
unapungua kama hivi sasa mnavyoona maji yamepungua.” Alisema.
Bw.
Kamote aliwaasa wananchi kuacha kuaharibu mazingira kwani athari zake
ni kubwa katika kuendesha mitambo ya kufua umeme ambao ni muhimu kwa
uchumi wanchi.“Yawezekana wanafanya shughuli hizo kwa kutokujua athari
zake katika uzalishaji umeme, kwa hivyo tunashauri wananchi waelewe
kwamba hilo ni tatizo na waache.” Alisetoa rai Bw. Kamote.
Naye
Kaimu Meneja wa Kituo cha kuzalisha umeme wa maji Mtera, Mhandisi David
Myumbilwa, ambaye kitaaluma ni Mhandisi wa Ujenzi, alisema lengo la
kuanzishwa kwa kituo hicho mwaka 1988 lilikuwa ni kutunza maji kwa ajili
ya kuendesha mitambo ya kufua umeme wa maji kwenye kituo cha Kidatu
mkoani Morogoro kabla ya kuongeza matumizi ya kituo hicho na kufanya
kazi zote mbili kufua umeme na kutunza maji (water storage).
“Kidatu
ndio kilikuwea kituo lengwa cha kufua umeme wa maji wakati huo, lakini
baada ya wataalamu kuona maji yanayotumika kwa kazi hiyo ni kidogo
ukilinganisha na mashine zilizokuwepo pale ikaonekana upo umuhimu wa
kutengeneza storage ya maji hapa Mtera na bwawa hili ndio kubwa kabisa
katika mabwawa ya kufua umeme wa maji nchini.” Alisema Mhandisi
Myumbilwa.
Alisema, kiwango cha juu cha ujazo wa maji kwenye
bwawa hilo ambao unahitajika kwa ajili ya kuendesha mitambo ni 698.5
m.s.a.l na kiwango cha chini ni 690 m.s.a.l, chini ya hapo kwa usalama
wa mitambo lazima izimwe.Mhandisi Myumbilwa amesema, Bwawa hilo
linategemea maji kutoka mito mitatu, Mto Kizigo unaotoka mkoani Singida,
Ruaha Mkuu, na Ruaha ndogo.
“Mto Kizigo ni mto wa msimu wakati
wa kiangazi unakauka, Ruaha ni mto asili na hapo nyuma ulikuwa na
kiwango cha juu cha maji lakini hivi sasa maji hakuna kabisa, na huu
ndio mto mkubwa unaotegemewa na Kituo cha Mtera.” Alifafanua.
Kwa
upande wake, Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Bi. Leila Muhaji alisema
lengo la ziara hiyo, ni kuweapa uelewa wahariri ili kujionea juhudi za
TANESCO katika kuhakikisha vyanzo vya maji yanayozalisha umeme
vinatunzwa kwani umeme wa maji ndio umeme nafuu zaidi.
“Mtakumbuka
kwamba Mheshimiwa Naibu Waziri katika kipindi cha tunatekeleza alisema
baadhi ya mashine za kufua umeme wa maji zinatengenezwa na kama
zinatengenezwa maana yake haitatoa umeme kwa kiwango chake cha kawaida.”
Alisema.
Mtaalamu wa Mazingira wa Shirika la Umeme nchini TANESCO, Bw. Yusuf
Kamote, akielezea jinsi mabadiliko ya tabia nchi na shughuli za
kibinadamu zinavyoathiri bwawa la Mtera. Kushoto ni Mhandisi Myumbilwa
Wahariri wakiangalia jinsi moja kati ya mashine mbili za kufua umeme wa maji inavyofanya kazi
Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Bi. Leila Muhaji, (kushoto), akiwa na
wasimamizi wa chumba cha udhibiti mwenendo wa mitambio kilichoko chini
ya ardhi kwenye kituo cha kufua umeme wa maji Mtera.
Fundi wa umeme mdogo, Elisha Kamenya akiwa kazini.
No comments:
Post a Comment