Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
Mamlaka
ya Chakula na Dawa (TFDA) imepata cheti cha mfumo wa uhakiki wa Ubora
wa Huduma cha Kiwango cha kimataifa cha ISO 9001.2015 na kufanya
mamlaka hiyo kuwa ya pili katika nchi zilizo kusini mwa Jangwa la
Sahara.
Akizungumza
katika uzinduzi huo Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto, Dk. Faustine Ndugulile amesema kuwa mafanikio ya TFDA
ni kutokana na kazi wanayofanya katika udhibiti dawa na chakula kwa
ajili ya kutumia bidhaa zenye ubora.
Amesema
kuwa TFDA ni mamlaka ambayo inagusa masilahi ya kila mtu na hakuna
asiyetumia bidhaa zinazodhibitiwa na mamlaka hiyo ikiwa ni kulinda afya
za wananchi ambao wanaweza kufanya kazi na kuiletea taifa maendeleo
hususani katika ujenzi wa uchumi wa viwanda.
Dk.
Ndugulile amesema kuwa TFDA kuimarisha udhibiti wa ubora na usalama wa
chakula, vipodozi, vifaa tiba na vitendanishi ni utekelezaji wa vitendo
wa azma ya serikali ya awamu ya tano chini uongozi mahiri wa Rais Dk.
John Pombe Magufuli katika kuhakikisha upatikanaji wa wa huduma bora za
afya hususani upatikakanaji wa dawa , vifaa tiba na vitandanishi.
Aidha
amesema nyenzo zilizofanya mafanikio katika udhibiti ni maamuzi ya
menejimenti zaidi ya miaka 10 wa kudhamiria kutekeleza mfumo wa uhakiki
ubora wa huduma .
Nae
Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Hiiti Sillo amesema kuwa katika kuongeza
huduma za udhibiti kwa wananchi wameanzisha ofisi saba za kanda ambazo
zitahudumia katika mikoa iliyopo katika kanda hizo.
Sillo
amesema kuwa mamlaka imekuwa ikitekeleza mfumo wa uhakiki ubora kuanzia
mwaka 2005 baada ya kufanya tathimini ya namna bora ya kufanya shughuli
za udhibiti kwa ufanisi na kutoa huduma bora kwa wateja.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula, Dawa
na Vipodozi (TFDA) Hiiti Sillo wakiwa wameshishika cheti cha mfumo wa
Uhakiki Bora katika Kiwango cha Kimataifa Cha Iso 9001-2015.
Meneja
Uchunguzi wa Dawa na Vipodozi Dkt. Yonah Hebron akitoa maelekezo mbele
ya Naibu Waziri Dkt. Faustine Ndugulile wakati akitembelea maabara
katika viunga vya Mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam, kulia kwa Naibu
Waziri ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula, Dawa na Vipodozi
(TFDA) Hiiti Sillo.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Chakula, Dawa na Vipodozi (TFDA) Hiiti Sillo (wakatikati) na Mwenyekiti
wa Bodi ya TFDA Dkt Ben Moses.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile akiwa kwenye piha ya pamoja wakati akizindua CHETI
CHA MFUMO WA UHAKIKI UBORA WA HUDUMA KATIKA KIWANGO CHA KIMATAIFA CHA
ISO 9001-2015 tukio lililofanyika katika viunga vya Mamlaka hiyo jijini
Dar es Salaam.




No comments:
Post a Comment