MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA MJI WA MAKAMBAKO HANANA MFIKWA AKITETA JAMBO NA MFADHILI HUYO BWANA ISDORY L.MWELADZI MAARUFU KAMA MUYAHUDI BAADA YA KUWASILI MEZA KUU.
MTENDAJI KATA YA UTENGULE JOB LUPONELO FUTE AKISOMA RISALA FUPI YA MGENI RASMI AKIWA NA AFISA ELIMU KATA YA UTENGULE.
DIWANI WA KATA YA UTENGULE STEPHAN MGOBA AKITOA NENO LAKE LA SHUKRANI KWA MAMBO WALIOSAIDIWA NA BWANA MWELADZI.
MUYAHUDI AKINONG'ONEZWA JAMBO LA MZEE MWENZAKE HAPA WANANG'ATANA SIKIO.
MWENYEKIJI WA KIJIJI CHA UTENGULE AKIFUNGUA MKUTANO ULIYOFANYIKA JANA KATIKA KIJIJI CHAKE CHA UTENGULE.
HITRA BENJAMINI MSOLA KATIBU WA ITIKADI NA UENEZI WILAYA YA NJOMBE AKIZUNGUMZA MBELE YA MKUTANO HUO WA UTENGULE.
BAADHI YA WADAU AMBAO NI WANANCHI WA UTENGULE WAKITETA JAMBO HAPA KWA FRAHA KUBWA.
WAZEE HAWA NAO WALIFIKA KUSHUHUDIA UTOLEWAJI WA PESA KUTOKA KWA MWANANCHI MWENZAO ISDORY MWELADZI MAARUFU KAMA MUYAHUDI WAKO PEMBENI KABISA NA KUNDI LA WANANCHI WALIOKUSANYIKA.
MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA MJI WA MAKAMBAKO HANANA MFIKWA AKIZUNGUMZA BAADA YA KUTOA AKAUNTI ZA BENKI ZA VIJIJI KWAMBA MDAU HUYO AMESAIDIA SERIKALI PALE AMBAPO HALMASHAURI ILITAKIWA KUCHANGIA SASA AMESAOIDIA YEYE NA KUOMBA NA WADAU WENGINE KUIGA MFANO HUO.
HUYU NI KAKA YAKE NA MFADHILI MUYAHUDI ANAFAHAMIKA KWA JINA LA MWALIMU ANJAWE L. MWELADZI MAARUFU KAMA MKALI AKIZUNGUMZA NA KUTOA NASAHA ZAKE.
WAKAZI WA KATA HII PIA NI WAJASILIAMALI WANAJISHUGHULISHA NA KILIMO CHA MBOGAMBOGA KAMA UNAVYOONA.
FRAHA IOJE KWA HAWA WAKAZI WA KATA HII TAZAMA BURUDANI HII
ANAITWA JENIFER AMBAYE YUKO KATIKA SHULE YA MSINGI UTENGULE NAYE KWA FRAHA ANAWAPIGIA GITAA
ALIYESIMAMA NA FIMBO NI DADA YAKE NA MFADHILI HUYO BWANA MUYAHUDI
NJOMBE
Zaidi Ya Shilingi Milioni Hamsini Zinatarajiwa Kuingizwa Kwenye Akaunti Za Benki Za Vijiji Vya Kata Ya Utengule Kuanzia Alhamishi Wiki Hii Kwaajili Ya Kuanza Utekelezaji Wa Miradi Mbalimbali Ikiwemo Zahanati Na Miradi Ya Maji.
Hayo Yamesemwa Na Mdau Wa Maendeleo Wa Kata Ya Utengule Isdory Mweladzi Maarufu Kama Muyahudi Mbele Ya Uongozi Wa Halmashauri Ya Wilaya Ya Njombe Ukiongozwa Na Mwenyekiti Wa Halmashauri Ya Mji Makambako Katika Siku Ya Kukabidhiwa Fedha Zilizoahidiwa Mwezi Mmoja Uliopita.
Bwana Mweladzi Amesema Pamoja Na Changamoto Mbalimbali Ambazo Zimekuwa Zikijitokeza Kwa Wananchi Amelazimika Kurudi Nyumbani Kwake Ambako Ni Kata Ya Utengule Kusaidiana Na Wananchi Katika Shida Na Raha Huku Akiomba Na Wadau Wengine Wa Maendeleo Kujitokeza Kusaidia Baadhi Ya Miradi Katika Kata Hiyo.
Bwana Mweladzi Amekemea Pia Tabia Za Baadhi Ya Viongozi Kutumia Fedha Za Serikali Na Zile Zinazotolewa Na Wafadhili Kutumia Kwa Maslahi Yao Binafsi Kwamba Asiwepo Mtu Wa Aina Hiyo Kwani Iwe Kanisani, Maofisini Fedha Zinakuwa Haziko Salaama.
Muyahudi Amesema Bado Atasaidia Pia Kukarabati Tenk La Maji La Kijiji Cha Utengule Ili Wananchi Wa Kata Hiyo Waepukane Na Changamoto Ya Kukosekana Kwa Maji Huku Zahanati Ya Kijiji Cha Utengule Ambako Amezaliwa Na Kusoma Hapo Akiahidi Kuiezeka Mwenyewe Ili Michango Ipunguzwe Kwa Wananchi.
Mwenyekiti Wa Halmashauri Ya Mji Wa Makambako Hanana Mfikwa Amepongeza Kwa Juhudi Na Moyo Aliyonao Mfadhili Huyo Kwa Msaada Wake Huku Akiwataka Viongozi Wa Kata Hiyo Kuanza Mchakato Wa Manunuzi Ili Miradi Ianze Kutekelezwa Kwa Haraka Na Kuhakikisha Fedha Hizo Zinafanya Kazi Iliyokusudiwa.
Afisa Mtendaji Wa Kata Ya Utengule Job Fute Akisoma Taarifa Ya Kata Ameshukuru Mfadhili Huyo Kwa Kutoa Misaada Mbalimbali Ikiwemo Kusaidia Ujenzi Wa Zahanati,Ofisi,Shule Na Kanisa Huku Diwani Wa Kata Hiyo Stephano Mgoba Akiahidi Ushirikiano Mkubwa Kusimamia Maendeleo Ya Vijiji Na Kata.
Mdau Huyo Wa Maendeleo Bwana Mweladzi Maarufu Kwa Jina La Muyahudi Tangu Mwanzo Ameonekana Kusifika Kwa Kusaidia Shughuli Mbalimbali Katika Kata Hiyo Ambayo Amezaliwa Hapo Ikiwemo Kuingiza Umeme Uliopo Kijiji Cha Ikelu Kwa Gharama Zake Lengo Kufikisha Shule Ya Sekondari Mtimbwi.
No comments:
Post a Comment