Waziri
wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla amefanya ziara maalum
kukagua masuala mbalimbali ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro sambamba
na kuzungumza na viongozi wa Mamlaka hiyo kwenye eneo la makao makuu
yake yaliyopo ndani ya hifadhi.
Katika
ziara hiyo, Waziri Dkt. Kigwangalla ameweza kupokea kupokea maoni na
masuala mengine ya kuendeleza Mamlaka hiyo ya Ngorongoro. Waziri yupo
Ngorongoro kwa muda wa siku mbili ambapo pia amepata kutembelea maeneo
ya hifadhi yenye migogoro na wafugaji.
Waziri
wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla akipokelewa na viongozi
wa Ngorongoro wakati alipowasili kwenye makao makuu ya hifadhi ya
Ngorongoro leo Oktoba 25, 2017.
Waziri
wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla akipata maelezo kutoka
kwa viongozi wa hifadhi hiyo wakati alipowasili kwenye makao makuu ya
hifadhi ya Ngorongoro leo Oktoba 25, 2017.
Waziri
wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla akipata maelezo kutoka
kwa mhifadhi wa Ngorongoro wakati alipowasili kwenye makao makuu ya
hifadhi ya Ngorongoro leo Oktoba 25,2017
Waziri
wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla akisikiliza maoni kutoka
kwa viongozi wa hifadhi ya Ngorongoro wakati alipowasili kwenye makao
makuu ya hifadhi ya Ngorongoro leo Oktoba 25,2017.
Mhifadhi
Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Freddy Manongi akizungumza
wakati wa kumkaribisha Waziri wa Maliasili Dkt.Kigwangalla alipowasili
hapo mapema leo kwa ajili ya kupata maelezo na ya kina namna ya
uendeshaji na masuala mbalimbali.
No comments:
Post a Comment