Wananchi
kutoka maeneo mbalimbali ya wilaya ya Arumeru mkoa wa Arusha
wakimsikiliza Mkuu wa idara ya Kilimo ya halmashauri ya Meru,Grace
Solomon kwenye kilele cha siku tatu za maonesho ya Jukwaa la Wakulima
Meru(Juwame) eneo la Leganga.
Meneja
kiongozi wa kampuni ya mbegu ya Monsanto nchini,Frank Wenga(kushoto) na
Mkuu Idara ya Kilimo katika halmashauri ya wilaya ya Meru mkoa wa
Arusha,Grace Solomon(katikati) wakimkabidhi zawadi ya baiskeli yenye
boksi maalumu la kubebea pembejeo mkulima bora kwenye maonesho ya
Wakulima na Wafugaji ya Nanenane mwaka huu kutoka mkoa wa
Kilimanjaro,Ebenezer Shao .
Mkulima
ambaye ameandaa mashamba darasa mengi kwaajili ya kutoa elimu kwa
wakulima wilayani Arumeru,Letayo Nnko akiwa na baskeli aliyokabidhiwa.
Meneja
kiongozi wa kampuni ya mbegu ya Monsanto nchini,Frank Wenga(kushoto) na
Mkuu Idara ya Kilimo katika halmashauri ya wilaya ya Meru mkoa wa
Arusha,Grace Solomon(katikati) wakimkabidhi zawadi ya baiskeli yenye
boksi maalumu la kubebea pembejeo mkulima bora kwenye maonesho ya
Wakulima na Wafugaji ya Nanenane mwaka huu kutoka mkoa wa Arusha,Kaanael
Kitomary .
Wananchi wakijifunza mbinu bora za kilimo kutoka kwenye mabanda yaliyoandaliwakuwahudumia wakulima.
Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja.
Arusha.Kampuni
ya mbegu ya Monsanto nchini imewatambua kwa kuwapa zawadi wakulima bora
watatu waliotangazwa washindi kwenye maonesho ya wakulima na wafugaji
ya Nanenane kanda ya Kaskazini yaliyofanyika kwenye viwanja vya Themi
jijini hapa mwezi Agosti mwaka huu na mkulima mmoja aliyeongoza kwa
kuandaa mashamba darasa.
Meneja
Kiongozi wa kampuni hiyo nchini,Frank Wenga alisema wameamua kutoa
zawadi za baiskeli zenye boksi maalumu la kubebea pembejeo wakati wa
kilele cha Jukwaa la Wakulima Meru (Juwame) baada ya kutambua uwezo wao
katika kilimo cha kisasa kinachozingatia kanuni za matumizi ya mbegu
bora.
"Kampuni
yetu inawapongeza kwa kuonesha mfano wa kuigwa katika mikoa
yenu,naamini wakulima wengine wataiga mbinu sahihi za kilimo mnazotumia
kufikia malengo hadi kutambuliwa kwenye maonesho ya kanda ya kaskazini
kama wakulima bora nasi tukiwa wadau tunawapongeza,"alisema Wenga
Walionufaika
na baiskeli hizo zenye thamani ya Sh 1.2 milioni ni mkulima bora kutoka
mkoa wa Kilimanjaro ni Ebenezeri Shao,Kaanael Kitomari kutoka mkoa wa
Arusha, Boay Tlem mkoa wa Manyara na Letayo Nnko mkulima kutoka
halmashauri ya Meru ambaye ameandaa mashamba darasa mengi zaidi kwaajili
ya kutoa elimu kwa wakulima wenzake.
Akizungumza
baada ya kukabidhiwa baiskeli hiyo,Nnko alisema itamsaidia katika
shughuli za kilimo na kuishukuru kampuni ya Monsanto kwa kutambua juhudi
zake za kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa usalama wa chakula.Awali
Mkuu wa idara ya kilimo katika halmashauri ya Meru,Grace Solomoni
alisema wakulima wamekua wakipata changamoto ya kupata mbegu bora kwa
wakati na wakati mwingine wamejikuta wakinunua mbegu bandia na kupata
hasara.
Aliwataka
wafanyabiashara wa makampuni ya mbegu kuhakikisha wakulima wanapata
mbegu bora kwa wakati ili kuwawezesha kuwa na kilimo chenye tija na sio
kulima kwa mazoea kwaajili ya kujikimu tu.






No comments:
Post a Comment