Ibada
ya uzinduzi na ufunguzi wa kanisa hilo imehudhuriwa na mamia ya waumini
wa kanisa hilo kutoka ndani na nje ya mkoa wa Shinyanga,ambapo askofu
Kezakubi pia alihubiri katika Ibada ya Jumapili katika kanisa hilo.
Akizungumza
kanisani hapo,Askofu Kezakubi aliwataka viongozi na waumini wa kanisa
hilo kutumia jengo hilo kwa ajili a ibada na siyo vinginevyo.“Nimefungua
kanisa hili mlitumie kwa ajili ibada,pia kuwaita watu wengine waje
kusikia neno la mungu ,sitaki kusikia mnatumia nyumba hii ya ibada
kutukanana na kufanya mambo yasiyompendeza Mungu”,alieleza Askofu
Kezakubi.
“Ni
aibu kusikia kelele kwenye kanisa,watu kutukanana kwene nyumba ya
Mungu,kama kuna mabaraza yanafanyika kanisani basi yafanyike kama
ibada,vivyo hivyo upande wa kwaya,sitaki kusikia mtu anatukuzwa
kanisani,mwenye kutukuzwa ni Mungu pekee”,aliongeza Askofu Kezakubi.
Katika
hatua nyingine alisema mchungaji ndiye mwalimu na msimamizi mkuu wa
masuala ya kiroho hivyo kuwataka wachungaji kufanya kazi yao vyema kwa
kuepuka kuwa wavivu na kutolegea kuwaombea na kuwatembelea waumini.
Askofu Kezakubi alitumia fursa hiyo
kuwatahadharisha baadhi ya watu wanaopinga viongozi wa dini kwenye
makanisa kuacha tabia hiyo kwani wanakwamisha kazi ya Mungu huku
akiwataka viongozi na waumini kushikamana katika kumtumikia Mungu.
"Kuna watu wapo kwenye makanisa yetu kwa bahati mbaya,wakiingia kanisani wanaanza vita badala ya kuwaunga mkono viongozi wao ili wafanye kazi yao vizuri,wakristo mnatakiwa pia kuwatunza watumishi wa mungu,tuwatunze watu waliolitumikia kanisa kwani tusipowatunza tunakosa baraka",alieleza Askofu Kezakubi.
Aidha aliwataka viongozi wa kanisa hilo kuiombea serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na rais John Pombe Magufuli ambaye amekuwa mstari wa mbele kukemea vitendo viovu. "Wakristo mnapaswa kumtii mungu,tuenende katika maisha anayotaka bwana,tusimame imara na kukataa mambo mabaya,kama mtu ataliharibu hekalu la Mungu,Mungu atamharibu mtu huyo",alisema.

Akisoma
risala Mwalimu Lucas Matanya alisema Kanisa la AICT Mto Jordani
lilianzishwa Novemba 13,2013 chini ya Mwinjilisti Nicodemus Lufega
likiwa na wakristo 7 wakisali chini ya mti na baadae idadi iliongezeka
kidogo wakajenga banda ambapo waliendelea na ibada katika eneo la Lugela
mtaa wa Shunu mjini Kahama.
“Kanisa
hili limekuwa tawi la AICT Kahama Mjini na kwa ushirikiano
uliopo,walinunua eneo na kuanza kujenga jengo hili la kuabudia na nyumba
ya kichungaji,choo na kuweka uzio,lengo likiwa ni kuhakikisha wanapata
huduma za kiroho karibu na makazi yao”,alieleza.
Aidha
alisema Baraza la Utumaji la Dayosisi ya Shinyanga limemtuma Mchungaji
Daudi Kazimoto kuwa mchungaji kiongozi wa kanisa la AICT Mto Jordan.
Alizitaja
changamoto zinazolikabili kanisa hilo kuwa ni ukosefu wa fedha kwa
ajili ya kununulia eneo ili kupanua eneo la kanisa kwani lililopo ni
dogo lakini pia ukosefu wa jengo la utawala.
Waumini wa kanisa la AICT Mto Jordan wakishuhudia zoezi la ufunguzi wa kanisa hilo
Waumini wa kanisa hilo wakishuhudia zoezi la uzinduzi wa kanisa hilo
Askofu Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Silasi Kezakubi akizungumza wakati wa uzinduzi wa kanisa hilo
Askofu Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Silasi Kezakubi akikata utepe
Askofu Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Silasi Kezakubi akisoma maandishi baada ya kukata utepe
Askofu
Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Silasi Kezakubi
akifungua kufuli ili aingie kwenye kanisa jipya la AICT Mto Jordan
Askofu Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Silasi Kezakubi akiingia kanisani
Askofu Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Silasi Kezakubi akiingia kanisani
Askofu Mkuu wa Kanisa la African Inland
Church Tanzania (AICT) Silasi Kezakubi akiwapungia mkono waumini wa
kanisa la AICT walioingia katika kanisa la AICT Mto Jordan
Askofu
Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Silasi Kezakubi
akiongoza ibada fupi ya ufunguzi wa kanisa la AICT Mto Jordan
Askofu Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Silasi Kezakubi akiongoza ibada katika kanisa la AICT Mto Jordan
Viongozi mbalimbali wakiwa kanisani
Muonekano wa kanisa la AICT Mto Jordan
Muonekano wa kanisa la AICT Mto Jordan
Kiongozi wa Ibada ya Jumapili leo Oktoba 15,2017,Mchungaji Adam Nzoka akizungumza baada ya uzinduzi wa kanisa la AICT Mto Jordan
Mchungaji
Elias Buluba kutoka kanisa la AICT Kahama Mjini akizungumza wakati wa
ibada katika kanisa la AICT Mto Jordan baada ya uzinduzi wa kanisa la
AICT Mto Jordan
Waumini wa kanisa hilo wakifuatilia ibada
Viongozi
wa kanisa la AICT wakisali wakati wa ibada ya Jumapili. Kulia ni
mchungaji kiongozi wa kanisa la AICT Mto Jordan,mchungaji Daudi
Kazimoto,katikati ni Makamu wa Askofu kanisa la AICT Dayosisi ya
Shinyanga,Aron Malyuta na kushoto ni Mchungaji Adam Nzoka

Kaimu Katibu Mkuu wa kanisa la AICT Dayosisi ya Shinyanga ,Mchungaji Timoth Shadrack akitambulisha wageni mbalimbali waliohudhuria zoezi la uzinduzi wa kanisa la AICT Mto Jordan

Mchungaji Simon Temu kutoka kanisa la AICT Ngudu mkoani Mwanza akijitambulisha

Makamu wa Askofu wa kanisa la AICT Dayosisi ya Shinyanga,Mchungaji Aron Malyuta akitoa neno wakati ibada ya Jumapili katika kanisa la AICT Mto Jordan

Viongozi wa kanisa la AICT wakiwa wamesimama kabla ya Askofu Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Silasi Kezakubi hajaaza kuhubiri neno la Mungu katika kanisa la AICT Mto Jordan
Kikundi cha sifa wakiimba wimbo wa kuabudu

Askofu Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Silasi Kezakubi ambaye ndiye Mlezi wa kanisa la AICT Dayosisi ya Shinyanga akitoa mahubiri wakati wa Ibada ya Jumapili katika kanisa la AICT Mto Jordan baada kuzindua kanisa hilo
Askofu Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Silasi Kezakubi akiendelea na mahubiri

Askofu Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Silasi Kezakubi akimtambulisha Mchungaji Daudi Kazimoto kuwa ndiye mchungaji kiongozi wa kanisa la AICT Mto Jordan.
Askofu Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Silasi Kezakubi akieleza sifa za Mchungaji
Daudi Kazimoto ambaye amebobea katika neno la Mungu hivyo ana uweza
mkubwa wa kuongoza hilo na kuwataka waumini wa kanisa hilo kumpa
ushirikiano
Askofu Mkuu wa Kanisa la African Inland
Church Tanzania (AICT) Silasi Kezakubi akiongoza zoezi la mchango kwa
ajili kupanua eneo la kanisa la AICT Mto Yordan
Askofu Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Silasi Kezakubi akiongoza zoezi la changizo hilo
Kaimu Katibu Mkuu wa kanisa la AICT Dayosisi ya Shinyanga ,Mchungaji Timoth Shadrack akitambulisha wageni mbalimbali waliohudhuria zoezi la uzinduzi wa kanisa la AICT Mto Jordan
Mchungaji Simon Temu kutoka kanisa la AICT Ngudu mkoani Mwanza akijitambulisha
Makamu wa Askofu wa kanisa la AICT Dayosisi ya Shinyanga,Mchungaji Aron Malyuta akitoa neno wakati ibada ya Jumapili katika kanisa la AICT Mto Jordan
Viongozi wa kanisa la AICT wakiwa wamesimama kabla ya Askofu Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Silasi Kezakubi hajaaza kuhubiri neno la Mungu katika kanisa la AICT Mto Jordan
Askofu Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Silasi Kezakubi ambaye ndiye Mlezi wa kanisa la AICT Dayosisi ya Shinyanga akitoa mahubiri wakati wa Ibada ya Jumapili katika kanisa la AICT Mto Jordan baada kuzindua kanisa hilo
Askofu Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Silasi Kezakubi akimtambulisha Mchungaji Daudi Kazimoto kuwa ndiye mchungaji kiongozi wa kanisa la AICT Mto Jordan.
Kwaya kutoka AICT Kahama Mjini wakimwimbia Mungu
Viongozi wa Kanisa la AICT wakiwa katika Ibada ya Jumapili
Viongozi wa kanisa la AICT wakiwa katika ibada ya Jumapili
Waimbaji kutoka kwaya ya AICT Kahama Mjini wakiimba na kucheza
Waumini wa kanisa la AICT wakiwa katika ibada ya Jumapili
Kwaya ya Akina Mama wakiimba wakati wa ibada hiyo
Ibada inaendelea
Kwaya ya AICT Bethelehemu mjini Kahama wakiimba na kucheza
Kwaya ya AICT Majengo wakiimba na kucheza
Kwaya ya AICT Galilaya Mhongolo ikiimba
Kwaya ya AICT Nyakato ikiimba
No comments:
Post a Comment