



……………………………………………………………………………………………………….
Waziri waNchi, OfisiyaRais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. AngellahKairuki
(Mb) amewataka Watendaji wa Taasisi za Serikali kusimamia suala zima la
watumishi na wadau kupata mrejesho wa barua wanazozituma kwenye taasisi
zao.
Mhe. Kairuki ameyasema hayo leo
wakati wa kikao kazi na watumishi wa mkoa wa Morogoro kilichofanyika
katika ukumbi wa Manispaa ya Morogoro.
Mhe. Kairuki amesema kumekuwa na
malalamiko mengi sana ya watumishi na wadau kutopata mrejesho wa barua
wanazozituma kwenye taasisi za Serikali na hata wakijibiwa sio kwa
wakati.
“Tunataka barua zijibiwe mara tu
mzipatapo, hata kukiri kupokea pia ni mrejesho hivyo ni vema tukajibu
barua na kwa wakati”Mhe. Kairuki alisisitiza.
Aidha, Mhe. Kairuki amewaagiza
Watendaji hao kufanya ufuatiliaji wa mara kwa mara kwenye masija la za
ofisi zao ili kuboresha utoaji huduma kwa umma.
Amesema eneo la ofisi za Masijala
limekuwa likilalamikiwa kwa kiasi kikubwa kwa majalada kutoonekana na
kusababisha watumishi na wadau kutopata mrejesho.
“Tutoe mwongozo kwa watumishi wa
Masijala na tusiwaache bila kuwafuatilia kwani eneo hili limekuwa
likilalamikiwa sana. Ikiwezekana tufanye kaguzi za kushtukiza ili kuleta
ufanisi katika kazi” Mhe. Kairuki aliongeza.
Ameongeza kuwa ufuatiliaji pia ufanyike kwa kila Ofisa ambaye anakaa na jalada kwa muda mrefu bila kutoa mrejesho.
Mhe. Kairuki amekutana na
watumishi wa Mkoa wa Morogoro ikiwa ni mwendelezo wa ziara alizozipanga
kuzitekeleza mikoani kwal engo la kusikiliza kero za watumishi ili
kuweza kuzitafutia ufumbuzi na kuangalia ni namna gani ya kuweza
kuboresha utendaji kazi Serikalini.
No comments:
Post a Comment