KUSHOTO NI KAIMU MKURUGENZI WA KAMPUNI YA TANWAT DKT RAJEEV SINGH MWENYE KOTI LA SUTI NA WA UPANDE WA KULIA NI AFISA UTAWALA WA KAMMPUNI HIYO EDMOND MNUBI
HILI NSLO NI SHILIKA LINALOHUSIKA NA UTETEZI WA MAKUNDI YA WATU WENYE ULEMAVU WA NGOZI NA MACHO
DIWANI WA KATA YA RAMADHANI GEOGE MENZON SANGA AKIZUNGUMZA NAYE MBELE YA WAGENI HAO
HAWA NDIYO WALIOBUNI NA KUTENGENEZA MEZA HIZO LEADING STEND
AFISA UTETEZI WA SHIRIKA LA UNDER THE SAME SUN
NJOMBE
Kampuni Ya Tanwat Mjini Njombe Imekabidhi Meza 100 Zenye Thamani Ya Shilingi Milioni Tano Za Kusomea Wanafunzi Wenye Ulemavu Wa Ngozi Na Macho Kwa Shirika Lisilo La Kiserikali La Under The Same Sun Kwaajili Ya Kupeleka Mikoa Ya Kanda Ya Ziwa Ili Kuwapatia Wanafunzi Wenye Ulemavu Huo Nao Wanufaike Kama Wanafunzi Wa Shule Ya Msingi Kibena.
Akikabidhi Msaada Huo Kaimu Mkurugenzi Wa Kampuni Ya Tanwat Dkt Rajeev Singh Akitafisiliwa Rugha Na Afisa Utawala Edmund Munubi Amesema Kampuni Hiyo Itaendelea Kushikamana Na Jamii Katika Maeneo Mbalimbali Ikiwemo Kushiriki Uchangiaji Shughuli Za Maendeleo Ya Ujenzi Wa Zahanati, Kuchimba Visima Vya Maji Na Kusaidia Makundi Ya Watu Wenye Ulemavu Wa Ngozi Na Macho Pamoja Na Wazee.
Aidha Dkt Singh Amelipongeza Shirika La Under The Same Sun Kwa Kutambua Uwepo Wa Makundi Ya Watu Wenye Ulemavu Wa Ngozi Na Macho Na Kupigania Kuyasaidia Makundi Hayo Kudai Haki Kwa Jamii Na Serikali Za Watu Wenye Ualbino Huku Akisema Mwaka Jana Wameanza Kutoa Huduma Mbalimbali Kwa Wazee Wanaoizunguka Kampuni Hiyo.
Kwa Upande Wake Mkurugenzi Wa Shirika La Under The Same Sun Viky Ntetema Pamoja Na Kushukuru Kwa Msaada Uliotolewa Na Kampuni Hiyo Ya Tanwat Pia Ametaka Serikali ,Wananchi Na Taasisi Mbalimbali Kuimalisha Ulinzi Kwaajili Ya Watu Wenye Albino Pamoja Na Kuwajali Kwa Kuwapatia Mahitaji Mhimu Ikiwemo Elimu, Malazi Chakula Na Mavazi Wanayostahili Kuyavaa.
Afisa Utetezi Wa Watu Wenye Ulemavu Wa Ngozi Ambaye Nae Ana Ulemavu Huo Kondo Seif Amesema Wao Kama Albino Wamekuwa Wakikabiliwa Na Changamoto Mbalimbali Ikiwemo Ngozi Kukosa Rangi Asili Kwa Kuathilika Na Jua Huku Wengi Wao Wanapoteza Maisha Kutokana Na Kuugua Maradhi Ya Saratani Yayotokana Na Kuungua Kwa Ngozi Zao Na Kuta Watoto Wenye Tatizo Hilo Wapea Mavazi Ya Kutosha.
No comments:
Post a Comment