Taasisi
ya Josephat Torner Foundation inayojishughulisha na watu walemavu
wameiomba Serikali kusaidia uingizaji wa mafuta ya ngozi kwa watu wenye
albino nchini.
Hayo
yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa taasisi hiyo Josephat Torner alipokuwa
akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam ambapo
alibainisha changamoto mbalimbali zinazo wakabili watu wenye ualbino.
“Watu
wengi wenye ualbino wanaishi chini ya miaka 40 kutokana na kukosa mafuta
ya kulinda ngozi dhidi ya miale ya jua, mafuta hayo huwasaidia
kutoathilika na magonjwa ikiwemo kansa ya ngozi,” alisema Torner.
Torner
alisema kuwa mafuta ya ngozi kwa watu wenye ualbino yanauzwa kati ya
shilingi 30,000 na 40,000 kwa chupa ambapo mtu mwenye ualbino mmoja
anatumia wastani wa chupa tano kwa mwaka.Mkurugenzi huyo alisema
kuwa gharama ya mafuta hayo ni kubwa kwa watu wenye ualbino ambao wengi
wao wanaishi maisha ya chini na hasa wale wanaoishi vijijini ambao
hawawezi kumudu kuyapata na kununua mafuta hayo.
Aidha,
aliongeza kuwa kama Serikali itasaidia uingizwaji wa mafuta hayo na
kupunguza ushuru ili yaingie nchini kama madawa kupitia Bohari Kuu ya
Dawa (MSD) tofauti na hali ilivyo sasa ambapo yanatozwa kodi kama
vipodozi, hatua hiyo itasaidia kupunguza kwa kiasi kubwa kushuka bei
mafuta hayo na kuwafikia walengwa.
Kwa
upande wake, Mratibu wa taasisi ya Afrikan Albino Foundation kutoka
Netherland nchini Tanzania Bas Kreukniet amesema kuwa ikiwa Serikali
itashiriki katika uingizaji wa mafuta hayo kuna uwezekano wa mafuta hayo
kuuzwa shilingi 4,000 kwa chupa.
Aliongezea
kuwa ikiwa bei ya mafuta hayo itapungua itawasaidia watu wengi wenye
ualbino hasa wa kipato cha chini na wale waishio vijijini kutumia mafuta
hayo na kuwasaidia kujikinga na miale ya jua.
Hadi
sasa taasisi ya Afrikan Albino Foundation imeweza kuwasaidia watu wenye
ualbino wapatao 13,000 tangu waanze kuleta mafuta hayo nchini mwaka 2004
ambapo kila mwezi jumla ya chupa 5,200 huingizwa nchini kwa ajili ya
kuwasaidia watu wenye ualbino.
No comments:
Post a Comment