SHIRIKA la
Ndege la Etihad ambalo ni shirika la ndege la taifa katika falme za
kiarabu limemteua George Mawadri (Pichani)kuwa Mkurugenzi mpya wa
shirika hilo nchini Nigeria, ambapo atahusika na kusimamia shughuli za
usafiri wa ndege za Etihad na biashara ya usafari wa anga na kuimarisha
biashara hiyo nchini Nigeria
Mkurugenzi
huyo mpya amekuwa na uzoefu katika sekta hiyo ya usafirishaji. Amefanya
kazi katika Shirika laNdege la British Airways kwa miaka 19 akiwa
nchini Uganda, Kenya na Zambia pamoja na kutoa huduma katika nchi za
Zimbabwe, Malawi, Ethiopia, Rwanda, Sudan na Sudan Kusini.
Nimefurahia
uteuzi kwenye nafasi hiyo muhimu katika Shirika Ndege la Etihad katika
sehemu ya sekta ya anga inayokuwa kwa kasi” Alisema Mawadri. Nitafanya
kazi kwa ushirikiano na kuwa mbunifu ili kuongeza ufanisi katika shirika
letu, kupanua masoko na kuwapa wateja wetu huduma bora.
Makamu
wa Rais wa Shirika la Ndege la Etihad, Danny Barranger alisema “Nina
furaha na imani kwamba George ataongoza vyema timu yetu iliyopo Nigeria
ili kuongeza soko la biashara yetu nchini humo. Uzoefu wake kwenye
biashara hii na rekodi yake ya mafanikio katika sekta ya anga Afrika na
maeneo aliyofanya kazi ni jambo ambalo litamwezesha kuendeleza kuongeza
ufanisi katika shirika la Etihad ambalo liliona umuhimu wa kumuweka
katika nafasi hiyo.
Shirika
la Ndege la Etihad lilizindua safari zake kati ya Lagos na Abu Dhabi 1
Julai 2012 na hivi sasa kuna safari nne kwa wiki kwa kutumia ndege ya
Airbus A330-200 yenye uwezo wa kubeba abiria 254 ambapo daraja la kati
abiria 18 na daraja la uchumi abiria 236.
No comments:
Post a Comment