Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye akizungumza na
wadau wa Habari,Michezo na sanaa Mkoa wa Mbeya (hawapo pichani)katika
ukumbi wa Mikutano wa Mkapa jijini Mbeya April 2 ,2015 .(Picha Keneth
Ngelesi)
Wadau wa
Habari,Michezo na Sanaa Mkoani Mbeya wakimsikiliza kwa makini Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye wakati wakati
akizungumza nao katika ukumbi wa Mikutano wa Mkapa jijini Mbeya.
Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye (kushoto) akipokea
taarifa ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali zinazo husu michezo,sanaa
,burudani kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makala katika mkutano
maalumu uliowakutanisha ,wadau wa michezo ,sanaa na burudani Mkoa wa
mbeya pamoja na baadhi ya viongozi wa halmashauri za mkoa wa Mbeya na
Songwe.
Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye akimkabidhi Ipadi
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amosi Makala kwa ajili ya Maafisa Habari wa Mkoa
wa Mbeya na Songwe katika kikao maalumu kilichowakutanisha wadau
mbalimbali wa Habari,sanaa,Michezo,kilichoitishwa na Waziri huyo kwa
lengo la kujadili changamoto na mafanikio ya sekta hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Chiku Galawa akizungumza katika mkutano huo.
Waziri wa
Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye amesema uamuzi wa
serikali kuzuia matangazo TBC kutokurusha moja kwa moja(live) matangazo
ya Bunge ilikuwa na lengo la kulinusuru shirika hilo lisife kwani
lilikuwa likitumia fedha nyingi kwa ajili ya matangazo hayo .
Amesema
uamuzi huo ni mkakati wa kuliwezesha shirika hilo kuweza kujiendesha
kwani awali lilikuwa likitumia fedha nyingi kwa urushaji wa matangazo ya
bunge bila ya malipo.Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo,
Nape Nnauye, amesema hayo jijini Mbeya, wakati akizungumza na wadau wa
habari,michezo, utamaduni na watendaji wa serikali Mkoa wa Mbeya na
Songwe,
Amesema
Shirika la utangazaji TBC, lilikuwa linaagizwa kurusha matangazo ya
bunge bila ya malipo ambapo kwa mwaka shirika lilikuwa likitumia Bilioni
4 kwa mapato yake ya ndani na kulifanya kushindwa kukarabati mitambo
pamoja na mslahi ya watumishi hivyo hivyo uamuzi huo ulikuwa sahihi
licha ya wengi kuonesha kutolidhishwa nalo.
Amesisitiza
kuwa suala hilo litaleta heshima ya Bunge kwani ilifika wakati, baadhi
ya wabunge walikuwa wakitoa lugha za maudhi pamoja na kucheza sarakasi
mambo ambayo yalikuwa yakivunja heshima ya bunge.Amesema kutokana na
hatua hiyo Bunge lenyewe ndio limechukua dhamana ya kuanzisha Studio
yake hivyo kutoa fursa kwa Televisheni nyingine kurusha matangazo ya
moja kwa moja lakini kulingana na vigezo na masharti yatakayohalalishwa
na mamlaka hiyo husika.
Akizungumzia
sheria ya baraza la michezo ambayo imekuwa ikilitaja suala la michezo
ni hiari na si uchumi, Nape amesema kwa sasa serikali ipo katika
mchakato wa kuirasimisha sheria hiyo ili iendane na sera ya michezo
ambayo imeweka wazi kwamba michezo kuwa shughuli rasmi ya
kiuchumi.ambapo katika kikao hicho wajumbe walipata nafasi ya
kuwasilisha kero na changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo.
Aidha,
akijibu risala iliyotolewa na Chama cha waandishi wa habari Mkoa wa
Mbeya, ambayo ilimuomba kiongozi huyo kuhakikisha anausimamia mswada huo
wa habari katika kulinda maslahi ya wafanyakazi,Nape, aliwataka
waandishi wa habari kutambua kuwa maslahi yao wanayoyapigania kutoka kwa
waajiri wao, yanajibiwa kwenye mswaada wa sheria ya huduma wa vyombo
vya habari.
Alisema,
wakati ule ulikuwa ni mwishoni mwa Bunge lililopita hivyo kwa sheria na
kanuni za Bunge mswaada huo unatakiwa ukasomwe tena kwa mara ya kwanza,
kwa hiyo umefikia pahala pazuri, na kuhakikisha kwamba maslahi ya
waandishi wa habari mule ndani yamelindwa.
Pia,
Waziri huyo, aliongeza kuwa serikali inaangalia utaratibu wa kuvifuta
baadhi ya vyuo vinavyotoa elimu ya habari ambavyo havina sifa, kwani
vimekuwa vikitoa waandishi wa habari amaboa hawana sifa na kazi yao
imekuwa ni kuupotosha umma.
No comments:
Post a Comment