Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Sunday, April 3, 2016

TAARIFA KWA UMMA:RAIS MAGUFULI AFANYA UTEUZI WA WENYEVITI WA BODI YA WAKURUGENZI YA CHUO CHA USIMAMIZI WA WANYAMAPORI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII

TAARIFA KWA UMMA

Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amefanya uteuzi wa Wenyeviti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori – Mweka na Bodi ya Wakurugenzi ya Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI)

Katika uteuzi huo, Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amemteua Profesa Faustin K. Bee kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori MWEKA. na Profesa Apolinaria E. Pereka kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI).

Uteuzi huo ni kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia tarehe 14/3/2016.

Kufuatia uteuzi huo uliofanywa na Mhe. Rais, Waziri wa Maliasili na Utalii kwa mamlaka aliyonayo chini ya Sheria ya Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori Sura ya 209 kifungu cha 4(3) kikisomwa pamoja na Jedwali aya ya 2(1b) amewateua wafuatao kuwa Wajumbe wa Bodi ya Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori MWEKA kwa kipindi cha miaka 3 kuanzia tarehe 14/3/2016.

Wajumbe walioteuliwa ni;

Samwel Maganga, Professor of Wildlife Management Sokoine University of Agriculture, Morogoro.Amani Ngusaru, Country Director, Tanzania World Wildlife Fund for Nature (WWF), Dar es Salaam.Andrew Gguga Seguya, Executive Director/CEO of Uganda Wildlife Authority, Kampala.Jafari Kidegesho, Department of Wildlife University of Agriculture Morogoro.Zuher H. Fazal, Vice Chairman Tanzania Tourism Organization, TATO, Arusha.

Alexander N. Songorwa, Mkuu wa Chuo cha Mweka, Moshi Simon Mduma, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania – TAWIRI, Arusha,Hassan Mshinda, Director General COSTECH, Dar es Salaam.Fred Manongi, Mhifadhi Mkuu Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro. – NCAA,Allan Kijazi, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi Tanzania -TANAPA, Arusha.Herman W. Keraryo, Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori Wizara ya Maliasili na Utalii.

Aidha kwa mamlaka aliyonayo chini ya Sheria ya Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania TAWIRI Sura ya 260 kifungu cha 6(2) kikisomwa pamoja na Jedwali la 2 aya ya 1(c), Mhe. Waziri wa Maliasili na Utalii amewateua wafuatao kuwa Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania TAWIRI kwa kipindi cha miaka 3 kuanzia tarehe 14/3/2016:
Wajumbe wa walioteuliwa ni;

Ndelilio A. Urio, Profesa wa Sayansi ya Wanyama na Uzalishaji Chuo cha Kilimo Sokoine, Morogoro.Martin Loibooki, Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA.Allan Kijazi, Mkurugenzi Mkuu, Hifadhi za Taifa TANAPA, Arusha.Freddy Manongi, Mhifadhi Mkuu, Mamlaka ya Hifadhi ya. Ngorongoro – NCAA Simon Mduma, Mkurugenzi Mkuu, Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania TAWIRI, Arusha.Theresia Nkya, Principal Medical Research Scientist NIMRI, Tanga.

Revocatus Kurwijila, Professor of Food Science, Chuo cha Kilimo Sokoine Morogoro.
Hassan Mshinda, Mkurugenzi Mkuu, COSTECH, Dar es Salaam.Masound H. Mruke, Profesa, Idara ya Entomolojia na Nyuki, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.Geophrey Kirenga, Katibu Mtendaji, Southern Agricultural Growth Corridor of Tanzania SAGCOT, Dar es Salaam.

IMETOLEWA NA:
Maj. Gen. Gaudence S. Milanzi
KATIBU MKUU
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII

No comments:

Post a Comment