Askofu
E. A.Kalinga pamoja na mkewe Mch Christina A.Kalinga kwa pamoja
wakishuhudia muujiza wa mtoto aliye zaliwa Baada ya maombezi, katika
picha mtoto Baraka Peter Lugega akiwa amebebwa na Baba yake Bw. Peter
Legega ,pamoja na Mama yake Eva Katikati Wakiwa Kanisani.Baada ya Bw.
Peter Lugega kuponywa pepo la ulevi uliopindukia na mke wake aliyepoteza
Mimba sita na alikuwa hajawahi kunyonyesha mtoto lakini baada ya
kuombewa na kuponywa anashangaa sasa ananyonyesha mtoto aliyejifungua
baada ya maombezi hayo.
Maeneo
tulipo : Morogoro Road Kimara Temboni Wilaya ya Kinondoni kabla ya
Mbezi mwisho, Saranga,hatua chache utaona kibao chetu barabara
ni-Kushoto rangi ya blue bahari.
6: Huduma zetu Kanisani:- Jumapili asubuhi saa 2:00 -4:30 watu wote kujifunza neno la Mungu ,Sunday School.
;saa
4:30-5:30 kusifu na kuabudu na mambo mengine (ibada ya kawaida)
5:30-6:30 maombi ya udhihilisho wa nguvu ya Mungu katikati ya kusanyiko
(ibada) -kujazwa Roho Mtakatifu (watu wote) -kunena kwa lugha mpya(watu
wote) -kuponywa magonjwa mbalimbali (watu wote) -kufunguliwa vifungo vya
uovu vya asili,na laana mbalimbali za watu (watu wote) 2: Jumatano: Hii
ni siku ya watumishi kuwepo Kanisani kuanzia Saa 2:00 asubuhi hadi saa
12:00 jioni kwaajili ya :- -Ushauri wa mtu mmojammoja (Canseling)
-maombi ya kufungua vifungo vya uovu kwa watu mbalimbali na laana
Mbalimbali -kuombea wagonjwa na kuponywa -kusikia shuhuda mbalimbali kwa
watu Mungu alivyo watendea. 3: Ijumaa siku hii ya ibada inaanza saa
10:00- 12:00 jioni tunasifu na Kuabudu ,na kusikia neno la Mungu ,na
Maombi.
Napenda
kueleza kwa wale wenye mapenzi mema kwa huduma yetu .Sisi tumepata bure
Tunatoa bure watu hawa tunao wahudumia ,au tulio wahudumia si matajiri
ni watu wa kawaida kama umeguswa na huduma yetu unaweza kuchangia huduma
hii ili iwafikie watu wengi zaidi.
Namba zetu za simu unaweza kutuma chochote,au kwa mazungumzo nasi Voda: 0767919056 - Tigo:0712964258 Airtel :0692567672.
Askofu
E.A.Kalinga aliye simama upande wa kulia katika picha, wakiwa katika
picha ya pamoja na Wachungaji. Baada ya kuwabariki katika Kanisa la
Sinai Tanzania Mkoa wa Rukwa, Sherehe hiyo ilihudhuriwa na viongozi wa
Serikali pia ,aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga mjini Meja Mstaafu
Bahati Matala ambaye wameshikana mikono kwa furaha pamoja na viongozi wa
Kta ya Malangali Wilaya ya Sumbawanga Mjini wakiwa pamojana baadhi ya
niongozi wa Kanisa.
Baadhi
ya waumini ndani ya kanisa wakijifunza neno la Mungu kipindi cha Sunday
School ambacho kimekuwa chenye baraka sana ya watu kulijua neno la
Mungu kwa kina .
Askofu
E.A Kalinga pamoja na mke wake Mchungaji Christina Kalinga waliokaa
viti vya mbele pamoja na baadhi ya waumini wakiwa katika hafla ya pamoja
wakisherehekea baada ya ubatizo katika Kanisa hilo. Hili ni jambo
linalo leta furaha katika utumishi, baada ya kuwafundisha watu neno la
Mungu na kuelewa na kukubali kubatizwa.Math 28:19-20;Mark 16:15-16.
Waumini
waliobatizwa wakiwa katika picha ya pamoja na Askofu Kalinga na mke
wake Mchungaji Christina Kalinga , wakisherehekea baada ya ubatizo wao
uliofanyika kwa Mchungaji Sekela Mushi wa kanisa la Penuel lililoko Suka
-Kimara Dar es Salaam.
Askofu
E.A Kalinga akimbatiza Mmoja wa waumini waliokata shauri na kubatizwa
na askofu huyo wa kanisa la Sinai Dar es salaam kwa ubatizo wa maji
mengi (kuzamisha).
Askofu
.E.A.Kalinga kulia akiwa katika picha ya pamoja na wanachuo wenzake
wakati wa walipohitimu shahada ya Diploma, katika chuo cha Bibilia cha
The Oasis Healing Bible College, kilichopo nyuma ya jengo la ubungo
Plaza, karibu na stendi ya mabasi yaendayo mikoani hapa Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment