Rais
Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete ametembelewa na ujumbe kutoka Taasisi ya
Dkt. Agostinho Neto ya Angola jana jijini Dar es Salaam. Ujumbe wa
Taasisi hiyo unaoongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Ndugu Amarildo Da
Conceicao uko nchini kwa lengo la kufanya mahojiano na viongozi wa
Tanzania kwa lengo la kuhifadhi historia ya mpigania uhuru na muasisi wa
Taifa la Angola Dkt. Agostinho Neto.
Akimuelezea
Dkt. Agostinho Neto, Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete amemzungumzia
mpigania uhuru huyo kuwa mtu mwenye kuzungumza kwa sauti ya upole
lakini kiongozi makini, shupavu na mwenye uwezo mkubwa wa kifalsafa na
kifikra. Dkt. Kikwete amesema anakumbuka akiwa kiongozi wa wanafunzi
katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, walimualika Dkt. Neto kuja
kuzungumza na wanafunzi katika Darasa la Itikadi alipozuru nchini mwaka
1974. Mpigania uhuru huyo aliyembatana na mkewe mwenye asili ya kireno
aliulizwa swali na mwanafunzi mmoja, 'iweje yeye ni mpigania uhuru dhidi
ya watu weupe ilihali ameoa mwanamke mweupe?'.
Katika jibu lake, Dkt. Neto alisema, 'mapambano hayana rangi, hatupambani na watu weupe tunapambana na ukoloni, mtu mweupe anaweza kuungana nasi katika mapambano yetu hali kdhalika wapo wenzetu weusi wanaoungana na kusaidia wakolini dhidi yetu'.
Katika jibu lake, Dkt. Neto alisema, 'mapambano hayana rangi, hatupambani na watu weupe tunapambana na ukoloni, mtu mweupe anaweza kuungana nasi katika mapambano yetu hali kdhalika wapo wenzetu weusi wanaoungana na kusaidia wakolini dhidi yetu'.
Rais Mstaafu
amewapongeza Taasisi ya Agostinho Neto kwa jitihada inazochukua za
kuhifadhi historia ya mpigania uhuru na muasisi wa Taifa la Angola.
Amewakumbusha umuhimu wa kuhakikisha kuwa historia hiyo inarithishwa kwa
kizazi baada ya kizazi ili watambue tulipotoka, tulipo na tunapotakiwa
kwenda.
Ujumbe
wa Taasisi ya Neto pia umefanya mahojiano kama hayo na Mama Maria
Nyerere, Mke wa Baba wa Taifa, Mheshimiwa Salim Ahmed Salim, Waziri Mkuu
Mstaafu na Katibu Mkuu Mstaafu wa Umoja wa Nchi za Kiafrika (OAU) na
viongozi na watanzania mashuhuri ambao walishiriki kwa namna moja au
nyingine katika harakati za uhuru wa Angola.
Imetolewa na Ofisi ya Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne,
Dar es Salaam
No comments:
Post a Comment