Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Mhungo akizungumza na
wafanyakazi wa wizara ya nishati na madini na kufungua baraza la
wafanyakazi wa wizara yake katika ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti
wa Baraza la wafanyazaki wa wizara ya Nishati na Madini, Selina
Msumbushi akizungumza na wafanyakazi wa wizara ya nishati na madini na
kusoma mapendekezo ya wafanyakazi hao leo katika mkutano wa kufungua
baraza la wafanyakazi uliofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Julius
Nyerere jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi
ya wafanyakazi wa wizara ya Nishati na Madini wakiimba wimbo wa
Solidarity leo katika ufunguzi wa Baraza la wafanyakazi katika ukumbi wa
Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi
wa wizara ya Nishati na Madini wakimsikiliza Waziri wa Nishati na
Madini, Profesa Sospeter Mhongo wakati wa ufungunzi wa Baraza la
wafanyakazi jijini Dar es Salaam leo.Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.
WAZIRI
wa Nishati na Madini, Mhe. Sospeter Muhongo amelishauri Baraza la
Wafanyakazi wa Nishati na Madini kujikita katika kujadili mwelekeo wa
mapinduzi ya kiuchumi kwa kuifanya Tanzania kuwa nchi yenye viwanda.
Mhe.
Muhongo ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati akifungua Kikao
cha Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo, ambapo baadhi ya mambo
yaliyojadiliwa katika kikao hicho ni masuala ya usafiri kwa wafanyakazi
wa wizara hiyo, upandishwaji vyeo kwa wafanyakazi, mafunzo pamoja na
uhaba wa nafasi wa ofisi kwa wafanyakazi.
Kuhusu
suala la upandishwaji vyeo, Mhe. Muhongo amesema kuwa tayari yeye kama
Waziri alishafanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Wizara ili kuona namna
gani wafanyakazi wanapandishwa vyeo kulingana na elimu pamoja uwezo wao
kikazi ambapo alipendekeza kubadili mtindo wa upandishwaji vyeo uliopo
sasa kwani ni wa zamani.
‘’Sifa
za upandishaji vyeo kwa wafanyakzi ni vema ukabadilika pamoja na muda
wa utoaji vyeo, hivyo napenda kuwasisitiza kuwaangalia vijana tulio nao
kwani pale Wizarani tuna vijana wengi wazuri wenye uwezo mkubwa katika
kufanya kazi. Katika kikao hiki ni vema mkajadili namna gani mnawapa
kipaumbele vijana katika kuwapandisha vyeo vijana hawa,’’ alisema
Muhongo.
Kuhusiana
na uhaba wa nafasi za ofisi, Mhe. Muhongo alifafanua kuwa, ofisi nyingi
za Serikali ziko katika mfumo wa zamani, hivyo amelishauri Baraza hilo
kuona namna gani watabadilisha muundo wa ofisi ili watu wakae pamoja
katika eneo moja lililo wazi na kufanya kazi kuliko kila mtu kuwa na
sehemu yake ya kufanyia kazi hali inayosababisha ufinyu wa eneo na
uvivu.
Aidha,
Amewataka wajumbe wa Baraza hilo kujadili ni namna gani wanaweza
kubadilisha hali ya kiuchumi toka asilimia 7% hadi kufikia asilimia 8%
mpaka 10% ili kukuza uchumi wa nchi na kutokomeza umasikini.
‘’Jukumu
kubwa la Wizara ya Nishati na Madini ni kuhakikisha kuwa tunakuza
uchumi wa nchi kwa kuhakikisha kuwa kunakuwa na umeme mwingi wa bei
nafuu na wa uhakika, na kazi tuliyonayo hapa ni kuongeza uzalishaji wa
umeme toka Megawati 1400 hadi kufikia Megawati 5,000 mpaka 10,000 na
ikiwezekana hadi 15,000 baada ya miaka 10 ijayo’’, aliongeza Mhe.
Mhongo.
Kuhusu
suala la Mafunzo kwa wafanyakazi hao, Mhe. Muhongo amesisitiza kuwa
hakuna mtu anayekatazwa kupatiwa mafunzo kwa maana ya kuongeza elimu juu
ya jambo fulani, isipokuwa kuna utaratibu wa kwenda kusoma, ambapo
panapotokea umuhimu wa wafanyakazi kwenda kusomea mambo muhimu yenye
manufaa kwa umma nafasi hizo ni vema zikatolewa ili nchi iwe na wataalam
mbalimbali katika nyanja mbalimbali.
‘’Hii
Wizara inahitaji watu wasome na waelimike, hivyo tunahitaji watu wasome
na wawe wataalam katika maeneo mbalimbali ya kazi lengo likiwa ni
kuleta maendeleo ya nchi’’, Alisema Mhe. Muhongo.
Amegusia masuala ya Bajeti katika Wizara yake ambapo amefafanua kuwa zaidi ya asilimia 89.5/% ya bajeti itatumika katika kufanya shughuli za maendeleo ya n
No comments:
Post a Comment