Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari
jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na watumishi hewa waliopo katika
Manispaa za Mkoa wa Dar es Salaam. Amesema kuwa mchakato wa kuwatafuta
watumishi hewa wengine unaendelea katika manispaa za mkoa wake.
Picha na Avila Kakingo.
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
MKUU
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kuwa kazi ya kutafuta
watumishi hewa katika manispaa za jiji la Dar es Salaam bado linaendelea
baada kubaini njia chafu wanazotumia watumishi hewa hao.
Akizungumza
leo na waandishi habari ,Makonda amesema kuwa Mkoa wa Dar es Salaam ni
kioo kwa nchi hivyo jitihada zinaendelea ya kutafuta na kazi hiyo
itafanywa sekta kwa sekta.
Amesema
kuwa Wakuu wa Wilaya katika jiji la Dar es Salaam hakuna kufanya kazi
yeyote mpaka wamelize kutafuta watumishi hewa kwa kutumia malipo ya
watumishi kutoka taasisi za fedha
(Pay Row).
(Pay Row).
Makonda
amesema idadi ya watumishi hewa 71 aliowasilisha kwa Waziri wa Nchi
Ofisi ya Rais –Tamisemi, Georgre Simbachawene ni ndogo katika jiji la
Dar es Salaam hivyo kazi lazima iwe endelevu.
Amesema
kuwa watumishi Hewa hawawezi wakawa wanalipwa mshahara huku wanaofanya
kazi kwa moyo mmoja wanajisikia vibaya hivyo ni lazima watafutwe na
wachukuliwe hatua na vyombo vya dola.
Mkuu
Mkoa amesema kuwa kati ya watumishi hewa 71 ni watumishi 34 hewa
wamefunguliwa mashitaka katika mahakama mbalimbali kutokana kuchukua
fedha wasioifanyia kazi.
No comments:
Post a Comment