BAADHI YA MADAKTARI WAKIWA NA MKUU WA MKOA KABLA HAWAJAONDOKA KUELEKA HOSPITALI YA KIBENA LEO ASUBUHI
HAPA MKUU WA MKOA WA NJOMBE DKT REHEMA NCHIMBI WAKIPEANA MAWAZO NJE YA OFISI YAKE
MGANGA MKUU WA SERIKALI KUTOKA MAKAO MAKUU ATAIFA AKIWA AMEMUWAKILISHA NAIBU WAZIRI WA AFYA PROF.MOHAMED BAKARI
MWAKILISHI WA KUTOKA NHIF MAKAO MAKUU DKT FRANK LEKEY AKIZUNGUMZA
SAMWEL MGEMA MGANGA MKUU MKOA WA NJOMBE AKIZUNGUMZA MBELE YA MGENI RASMI AKISHUKURU KWA KUPEWA VIFAA TIBA KATIKA HOSPITALI YA KIBENA
MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA UKIKABIDHI VIFAA TIBA KWA MGANGA MKUU WA MKOA SAMWEL MGEMA NA YEYE KUMKABIDHI MGANGA MKUU WA HOSPITALI YA KIBENA
MWAKILISHI WA MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA KUTOKA MAKAO MAKUU NHIF DKT FRANK LEKEY
HAWA NI BAADHI YA WANANCHI NA WAGONJWA WALIOHUDHURIA KWENYE UZINDUZI HUO WA WIKI YAKUWA NA MADAKTARI BINGWA MKOA WA NJOMBE
Wananchi Mkoani Njombe Wameshauriwa Kujiunga na Mifuko ya Bima ya Afya Ikiwemo ya NHIF na HCF Ili Kukabiliana na Gharama za Matibabu Pindi Wanapokwenda Kutibiwa Katika Vituo Vya Afya na Hospitali Mbalimbali Nchini.
Rai Hiyo Imetolewa na Mwakilishi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya NHIF Makao Makuu Dkt Frank Lekey Wakati wa Uzinduzi wa Wiki ya Utoaji Huduma za Magonjwa Mbalimbali Yakiwemo Kinamama na Uzazi Yatakayotolewa na Madaktari Bingwa Katika Hospitali ya Mkoa wa Njombe Iliyoko Kibena
Akizungumzia Lengo la Serikali Kupitia NHIF Mganga Mkuu wa Serikali Profesa Mohamed Bakari
Amesema ni Kusongeza Karibu Huduma za Matibabu Kwa Wananchi Wanaohitaji Matibabu ya Madaktari Bingwa , Huku Mnganga Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dkt. Samuel Mgema Akishukuru Kwa Msaada wa Vifaatiba Walioupata
Akizungumza Kwa Niaba Ya Katibu Mkuu Wa Wizara Ya Afya,Maendeleo Ya Jamii,Jinsia ,Wazee Na Watoto Mgeni rasmi Mganga Mkuu Wa Serikali Kutoka Makao Makuu Taifa Profesa Mohamed Bakari Ambaye Amesema Serikali Ya Awamu Ya Tano Imedhamilia Kupeleka Huduma Za Afya Karibu Na Wananchi Mahali Wanapopatikana Ambapo Tayari Huduma Hizo Zimewafikia Wananchi Wa Mikoa 14 Nchini.
Profesa Bakari Amesema Dhamira Ya Wizara Ya Afya Kwa Kushirikiana Na Mfuko Wa Taifa Wa Bima Ya Afya Na Kuwataka Wananchi Nchini Kuongfeza Jitihada Za Kujiunga Na Mfuko Wa Bima Ya Afya Na Kusema Kuwa Kadri Miaka Inavyoendelea Huduma Za Matibabu Zitakuwa Ni Kubwa Na Hivyo Ili Kumudu Gharama Za Afya Ni Vema Kila Mmoja Kujiunga Na Mifuko Ya Bima Ya Afya.
Kuhusu Kundi La Wazee Pr. Bakari Ametaka Madaktari Kutoa Kipaumbile Kwa Wazee Katika Huduma Mbalimbali Ambazo Zitakuwa Zikitolewa Kwenye Hospitali Huku Akipongeza Mfuko Wa Taifa Bima Ya Afya Kwa Ushirikiano Mkubwa Ambao Wanautoa Katika Mkoa Wa Njombe Na Kuomba Wananchi Waunge Mkono Jitihada Za Mfuko Huo.
Kwa Upande Wao Baadhi ya Wagonjwa na Wananchi Waliohudhuria Uzinduzi Huo Wamesema Kuwepo Kwa Madaktari Bingwa Hao Karibu na Maeneo Yao Yamesaidia Kupunguza Gharama ya Kuwafuata Madaktari Bingwa Katika Hospitali za Rufaa Zilizo Nje ya Mkoa wa Njombe.
Madaktari Hao Bingwa Watano Kutoka Idara Tofauti Watakuwepo Katika Hospitali ya Mkao wa Njombe Kwa Siku Tano Wakitoa Huduma za Upasuaji wa Mfumo wa Mkojo, Nusu Kaputi, Usingizi na Wagonjwa Mahututi, Magonjwa ya Kinamama na Uzazi, Watoto Pamoja na Magonjwa ya Ndani na Moyo.
No comments:
Post a Comment