Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia), akisalimiana na Mjumbe wa Kamati
ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Mhe. Kangi
Lugola, wakati Kamati hiyo ilipotembelea Makao Makuu ya Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi. Kushoto ni mjumbe mwingine wa kamati hiyo, Juliana
Shonza.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Balozi Adadi Rajabu,
akiongoza kikao wakati Kamati hiyo ilipokutana na Viongozi na Watendaji
wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara
hiyo Meja Jenerali Projest Rwegasira.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama na Viongozi na Watendaji Wakuu
wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, wakiwa katika mkutano uliofanyika
katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi jijini Dar
es Salaam wakati Kamati hiyo ilipotembelea Makao Makuu ya Wizara hiyo.
Katikati meza kuu ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Balozi Adadi Rajabu na
kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, wakiongozwa na Mwenyekiti wa
kamati hiyo, Balozi Adadi Rajabu (wa tatu kulia), wakikagua mojawapo ya
samani za ofisi ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi, Balozi Simba Yahya, ambazo zimetengenezwa na Jeshi la Magereza,
wakati Kamati hiyo ilipotembelea Makao Makuu ya Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka
ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dk. Modestus Kipilimba, akizungumza
wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama,
ilipotembelea Makao Makuu ya Mamlaka hiyo, jijini Dar es Salaam kuona
shughuli mbalimbali zinazofanywa na Mamlaka hiyo. Wa kwanza kutoka
kushoto (waliokaa) ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
Meja Jenerali Projest Rwegasira na wa tatu ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo,
Balozi Adadi Rajabu.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya
Uzalishaji Vitambulisho wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA),
Alphonce Malibiche, akielekeza jinsi ya kutambua taarifa sahihi za
mwombaji wa kitambulisho cha Taifa kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (hawapo pichani), wakati Kamati
hiyo ilipotembelea Mamlaka hiyo, jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (katikati), akizungumza
na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na
Usalama, Balozi Adadi Rajabu (kushoto) mara baada ya Kamati hiyo
kumaliza ziara yake katika Makao Makuu ya Wizara hiyo na Mamlaka ya
Vitambulisho vya Taifa (Nida). Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara
hiyo, Balozi Simba Yahya.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira, akiagana na Mwenyekiti
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Balozi
Adadi Rajabu (kushoto), mara baada ya Kamati hiyo kumaliza ziara yake
Makao Makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na Mamlaka ya
Vitambulisho vya Taifa (NIDA). Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara
hiyo, Balozi Simba Yahya.(Picha na Wizara ya Mambo ya Nchi)
No comments:
Post a Comment