Mkuu
wa Mkoa wa Mbeya Amosi Makala akizungumza na wananchi wa kijiji cha
Luhanga Wilayani Mbarali Mkoani Mbeya kwa lengo la kutoa tamko la
serikali juu ya ulejeshwaji wa ardhi ya wananchi hao hekta 5000 ambazo
zilichukuliwa na wawekezaji.
Mkuu
wa Mkoa wa Mbeya Amosi Makala akisisitiza jambo katika Mkutano wa
hadhara ulioitishwa na Mkuu huyo wa Mkoa kwa lengo la kuzungumza na
wananchi wa kijiji cha Luhanga (Hawapo Pichani)Wilayani Mbarali Mkoani
Mbeya .
Baadhi
ya wananchi wa kijiji cha Luhanga Mbarali Mkoani Mbeya wakimsikiliza
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya katika mkutano wa hadhara ulioitishwa na Mkuu huyo
wa mkoa kwa lengo la kulejeshewa ardhi yao iliyochukuliwa na wawekezaji
.
Mkutano
ukiendelea katika kijiji cha Luhanga Mbarali katika ya Mkuu wa Mkoa wa
Mbeya na Wananchi wa kijiji hicho ambao walikuwa katika mgogoro mkubwa
wa ardhi na wawekezaji.
Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Mbeya Guram Shekifu akimshukuru Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makala mara baada ya kumaliza mgogoro huo.
Wananchi wakifuatilia Mkutano.
Baadhi ya watendaji wa halmashauri ya wilaya ya Mbarali Mbeya wakichukua kumbukumbu za Mkutano huo.
SERIKALI
Mkoni Mbeya, imezirejesha hekta 5000 za ardhi ya kijiji cha Luhanga
Wilayani Mbarali, zilizokuwa zimetolewa kwa wakulima zaidi ya 200 wa
chama cha Luhanga (Luhanga AMCOS), huku ikiuagiza uongozi wa halmashauri
kuwachukulia hatua watendaji wote walihusika na mchakato wa ugawaji wa
ardhi hiyo.
Akikabidhi
ardhi hiyo leo, kwa wananchi wa Kata ya Luhanga, Wilayani humo, Mkuu wa
Mkoa wa Mbeya, Amosi Makala, alisema serikali imefikia uamuzi huo baada
ya kubaini kwamba zoezi hilo lilifanyika kinyume na sheria na kanuni
za ardhi za vijiji zinavyoelekeza.
Amesema,
sheria mama namba 5 ya ardhi ya mwaka 1999, imebainisha kwamba
halmashauri ya kijiji haina mamlaka ya kugawa ardhi zaidi ya ekali 20 au
50 lakini wao wamegawa ardhi zaidi ya hekta 5000.
Mkuu
huyo ameongeza kuwa mbali na zoezi hilo kughubikwa na ukiukwaji wa
sheria lakini pia, wawekezaji hao wameonekana ni wababaishaji kutokana
na kushindwa kutimiza ahadi za maendeleo walizokuwa wamezitoa kwa
wananchi wa eneo hilo.
Aidha,
Makala, aliwatahadharisha wananchi hao, kujiepusha na walaghai wa ardhi
na kuacha kugawa ardhi ovyo kwani rasilimali hiyo haiongezeki
ukilinganisha na mahitaji ya watu, ambao kila siku wanaongezeka
idadi.Amesema serikali inaweza kufanya uparesheni ya kuwataka vijana
wafanye kazi lakini kama wananchi au viongozi wanauza ardhi zoezi hilo
haliwezi kufanikiwa .
Amesema
mkoa wa mbeya unajulikana kwa kuongoza kwa migogoro ya ardhi hususani
wilaya ya mbarali hivyo yeye kama mkuu wa mkoa atahakikisha
anashughulika vyema na suala hilo.Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa
Mkoa amezitaka jamii za wafugaji wa kimasai kuhakikisha wanaachana na
tabia ya kuozesha watoto wa kike katika umri mdogo badala yake
wawalitihishe katika elimu ambayo ndio mkombozi kwao.
Habari hii imeandaliwa na mtandao wa kijamii wa www.jamiimoja.blogspot.com-
No comments:
Post a Comment