Msemaji
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Christopher Ole Sendeka akizungumza na
waadishi wa habari leo, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM,Lumumba jijini
Dar es Salaam,leo.
Picha na Bashir Nkoromo)
…………………………………………………………………………………………………
Aliyekuwa mgombea Urais wa UKAWA
kupitia CHADEMA, Ndugu Edward Lowassa, Aprili 7, 2016 alifanya
mazungumzo na Wanazuoni kutoka katika vyuo vikuu vya ndani na nje ya
nchi.
Katika mazungumzo hayo, Ndugu
Lowasa aligusia masuala mbalimbali ya Kitaifa yakiwemo hali ya siasa
nchini, kuachisha kazi watumishi wenye tuhuma mbalimbali, na kile
alichokiita tatizo la mfumo nchini.
Alichokifanya Ndugu Lowassa ni
kutaka kuwaaminisha Watanzania masuala yasiyo sahihi kwa maslahi ya
kisiasa, kwani ukweli ni kwamba; Mosi, Rais John Pombe Magufuli hatafuti
umaarufu, badala yake yeye na Serikali yake wanachapa kazi ili
kuwaletea maendeleo Watanzania kwa ujumla.
Pili, kuhusu suala la mfumo,
Tanzania haina tatizo la kimfumo, kwani mifumo iliyopo, iliyowekwa tangu
awali na waasisi wa Taifa letu, Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage
Nyerere na Hayati Abeid Aman Karume ni imara na imekuwa ikiboreshwa
kulingana na mahitaji.
Ifahamike hakuna mahali popote
duniani ambako mfumo wa nchi unajiendesha wenyewe, siku zote mfumo
huongozwa na kuendeshwa na binadamu ambao kwa udhaifu wa ama kibinadamu
au wa kukusudia, hufanya makosa yanayohitaji kusahihishwa kwa taratibu
zilizowekwa.
Tatu, Hakuna mtumishi aliyeachishwa au kusimamishwa kazi kwa sababu ya hali ngumu ya uendeshaji wa Shirika lolote, isipokuwa hatua hiyo imechukuliwa ili kupisha uchunguzi kutokana na tuhuma mbalimbali za ukiukaji na matumizi mabaya ya ofisi na madaraka, ubadhirifu, uhujumu uchumi na ufisadi.
Tatu, Hakuna mtumishi aliyeachishwa au kusimamishwa kazi kwa sababu ya hali ngumu ya uendeshaji wa Shirika lolote, isipokuwa hatua hiyo imechukuliwa ili kupisha uchunguzi kutokana na tuhuma mbalimbali za ukiukaji na matumizi mabaya ya ofisi na madaraka, ubadhirifu, uhujumu uchumi na ufisadi.
Chama Cha Mapinduzi kina ushahidi
wa utendaji wa Ndugu Lowasa akiwa Waziri Mkuu namna alivyoendesha zoezi
la kusimamisha na kufukuza kazi na kuwadhalilisha watumishi bila
kufuata taratibu, hali hiyo ni tafauti sana na hii ya sasa, kwani kila
anayesimamishwa kazi, anasimamishwa kwa kufuata taratibu zote, ili
kuhakikisha kila mtumishi anatendewa haki ya kusikilizwa.
Na katika hili la kuwasimamisha
kazi watumishi wa umma wanaotuhumiwa kwa ufisadi, wizi na matumizi
mabaya ya ofisi, Chama Cha Mapinduzi kitaendelea kuunga mkono, kutokana
na baadhi yao kuwa chanzo cha shughuli za maendeleo nchini.
Kiongozi au mwanasiasa
anayemkosoa Rais Magufuli katika hatua anazozichukua hivi sasa, ikiwa ni
pamoja na kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za umma, ni wa kutiliwa
shaka kwani kufanya hivyo ni sawa na kutetea wizi, ufisadi na uporaji wa
rasilimali za nchi.
Ndugu Christopher Ole Sendeka
MSEMAJI WA CCM
MJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA,
MSEMAJI WA CCM
MJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA,
08/04/2016
No comments:
Post a Comment