AFISA MAENDELEO WILAYA YA NJOMBE ABRAHAMU KAAYA AKIWA KWA NIABA YA MKURUGENZI WA HALMASHAURI HIYO
WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI KIDEGEMBYE WAKITUMBUIZA
UJUMBE WA WANAFUNZI HUO
JULIUS SALINGWA NI DIWANI WA KATA YA KIDEGEMBYE AKIAHIRISHA SHEREHE ZA WANAWAKE SIKU YA JANA
MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MAKAMBAKO AKISALIMIA WANANCHI
KATIBU TAWALA WILAYA YA NJOMBE AKITOA NASAHA KWA WAKINA MAMA WA KIDEGEMBYE
MWENYE NGUO NYEKUNDI KWENYE MEZA KUU NI MGENI RASMI MKUU WA WILAYA YA NJOMBE SARAH DUMBA
AKINA MAMA WAKIFURAHI KWA SHEREHE HIZO
DEBORA NSEMWA AKISOMA TAARIFA FUPI MBELE YA MGENI RASMI
MKUU WA WILAYA YA NJOMBE SARAH DUMBA AKIKABIDHI NDOO KWA WAHUDUMU WA ZAHANATI YA KIJIJI CHA KIDEGEMBYE
Mkuu Wa Wilaya Ya Njombe Bi.Sarah Dumba Ametaka Akina Mama Kufanya Kazi Kwa Bidii Kwaajili Ya Kujikwamua Kiuchumi Ili Kufikia Malengo Ya Kauli Mbiu Ya Mwaka Huu Inayosema Hamsini Kwa Hamsini Ifikapo 2030 Tuongeze Jitihada Ambapo Amesema Mifumo Dume Inatakiwa Kutokomezwa Katika Jamii.
Akizungumza Kwenye Maadhimisho Ya Kilele Cha Siku Ya Wanawake Mkuu Wa Wilaya Ya Njombe Sarah Dumba Amesema Mwanamke Anakabiliwa Na Changamoto Ambazo Zinaweza Kutafutiwa Ufumbuzi Ambapo Mfumo Dume Unaofanywa Na Baadhi Ya Wanaume Utamalizika Wanawake Wakiongeza Bidii Ya Kufanya Kazi.
Bi.Dumba Ametaka Wanaume Kuonesha Ushirikiano Na Mfano Wa Kuwasaidia Akina Mama Na Watoto Wakike Kuhakikisha Wanashiriki Kikamilifu Kwenye Fursa Mbalimbali Na Kuweka Uhuru Utakaowawezesha Kujituma Kufanya Kazi Ili Kuondokana Na Hali Ya Udhaifu Unaoonekana Kwa Wanawake.
Aidha Bi. Dumba Ameitaka Jamii Kuziacha Tamaduni Ambazo Zinamkandamiza Mwanamke Za Kukosa Haki Ya Kupata Urithi wa ardhi na Mali mbalimbali Katika Familia,Ukeketaji,Kulea Watoto Na Kuwatumikisha Kazi Za Ndani , Kudhalilishwa Kwa Kuwapiga Na Waume Zao Baada Ya Kuhitilafiana Huku Akisema Wanawake Ni Washiriki Wakuu Kwenye Kilimo Na Biashara.
Amesema Madhara Ya Mfumo Dume Ni Kurudisha Nyuma Maendeleo Ya Taifa Na Jamii Kwani Umesababisha Uwiano Kutofautiana Katika Kushika Nafasi Za Nyanja Mbalimbali Kwenye Ajira,Siasa,Elimu Na Shughuli Za Kibiashara Ambazo Idadi Kubwa Zimeshikwa Na Wanaume Ambapo Wanawake Wametakiwa Kuongeza Juhudi Za Kufanya Kazi.
Akisoma Taarifa Fupi Mbele Ya Mgeni Rasmi Afisa Maendeleo Ya Jamii Wilaya Ya Njombe B.Debora Nsemwa Amesema Halmashauri Inaadhimisha Siku Ya Wanawake Kwa Kuzingatia Sera Ya Maendeleo Ya Wanawake Na Jinsia Ya Mwaka 2000 Ambayo Inatoa Mwelekeo Kwa Jamii Kuhakikisha Inazingatia,Sera,Mipango,Mikakati Na Shughuli Za Maendeleo Kuzingatia Usawa.
Akiahirisha Sherehe Hizo Diwani Wa Kata Ya Kidegembye Julius Salingwa Pamoja Na Kushukuru Kwa Hotuba Iliyotolewa Na Mgeni Rasmi Lakini Amesema Akina Mama Haki Zao Zipo Pale Pale Hakuna Wakuzibadilisha Huku AKiwataka Wauguzi Wa Zahanati Ya Kijiji Hicho Kutunza Vyombo Vilivyotolewa Kwaajili Ya Matumizi Ya Zahanati Hiyo.
No comments:
Post a Comment