Mgeni Rasmi katika maadhimisho Mkuu wa mkoa wa dar-es-salaam Mhe. Paul makonda akihutubia waumini waliojitokeza changia damu
Wageni waalikwa katika maadhimisho hayo kutoka kushoto Meneja damu
salama kanda ya Mashariki Dr Aveline Mgasa, Mganga mkuu mkoa wa Dar ,
Dr Grace magembe, Mhe. Paul Makonda, Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dr Mpoki
Ulisubya.
Baadhi ya waumini wakichangia damu kwa hiari
Mpango wa Taifa wa Damu
salama kwa kushirikiana na waumini wa dhehebu la sabato wameendesha zoezi la
kuchangia damu katika mikoa mbalimbali hapa nchini, mikoa hiyo ni Mara, Kigoma,
Dar-es-salaam, Dodoma, Mwanza, Kilimanjaro,Tabora, Morogoro, Mbeya na Iringa.
Siku ya matendo ya huruma hufanyika jumamosi ya
tatu ya
mwezi wa tatu kila mwaka, ambapo waumini hushiriki katika huduma
mbalimbali za
jamii. Lengo ni kukusanya chupa za damu 3000 kutoka katika mikoa hiyo
ambazo zitasambazwa Hospitali mbali mbali kuokoa maisha ya wahitaji
No comments:
Post a Comment