Mkurugenzi
wa Idara ya Tawala za Mikoa kutoka TAMISEMI Bi. Suzani Chekani
akionesha katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati akiwasilisha
mada kuhusu kuwajibika kwa kuzingatia sheria za nchi kwa wakuu wa mikoa
wapya katika kikao kilichofika leo Jijini Dar es Salaam kulia ni Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)
Mhe. George Simbachawene.
Naibu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(TAMISEMI) Mhe. Suleiman Jafo akizungumza na wakuu wa mikoa(Hawapo
pichani) kuhusu suala la kutatua changamoto zilizopo katika mikoa katika
katika kikao kilichofika leo Jijini Dar es Salaam kushoto ni Waziri wa
Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe.
George Simbachawene.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)
Mhe. George Simbachawene akizungumza na wakuu wa mikoa (Hawapo pichani)
akiwataka kwenda kuwajibika kwa kwa kuzingatia sheria na kutatua
changamoto za wananchi katika mikoa yao katika kikao kilichofika leo
Jijini Dar es Salaam .
Baadhi ya wakuu wa mikoa wakifatilia maelekezo toka kwa Waziri wa Nchi
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe.
George Simbachawene (Hayupo pichani) katika kikao cha kuwakumbusha
majukumu yao kama wakuu wa mikoa.Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)
Mhe. George Simbachawene (kutoka wa tatu kulia) akiwa katika picha ya
pamoja na wakuu wa mikoa wapya walioapishwa jana kulia mwa Waziri ni
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(TAMISEMI) Mhe. Suleiman Jafo.
Picha zote na Raymond Mushumbusi MAELEZO
……………………………………………………………………………………………
Na Jacquiline Mrisho Maelezo
Waziri wa Nchi Ofisi ya
Rais,TAMISEMI, Mhe.George Simbachawene amewataka Wakuu wa Mikoa
walioapishwa kufanya kazi kwa bidii na kutumia muda mwingi kutatua kero
zinazowakabili wananchi katika maeneo yao.
Mhe.Simbachawene ameyasema hayo
leo Jijini Dar es salaam alipokutana na Wakuu hao wa Mikoa ambapo
amewasisitiza kwenda na kasi ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli ili
kutimiza malengo yaliyopangwa katika uongozi wa Serikali ya awamu ya
tano.
“Mfumo wa sasa wa uongozi ni
tofauti na mfumo wa zamani, namna Mhe. Rais anavyotaka tufanye kazi ni
tofauti na zama zingine zilizopita,Wakuu wa Mikoa mnapaswa kujua kila
kinachoendelea kila siku katika Mikoa yenu na mnapaswa muwajibike kwa
wananchi wenu”alisema Simbachawene.
Mhe.Simbachawene ameongeza
kuwa,Wakuu wa Mikoa wamepewa madaraka ya kusimamia mfumo wa ufanyaji
kazi kwa kuhakikisha watumishi wa umma wanawajibika ipasavyo kwakua nchi
haiwezi kubadilika kama hakutakua na utendaji mzuri.
Aidha,Mhe.Simbachawene
amewakumbusha Wakuu wa Mikoa wazingatie na kusimamia haki za wananchi
kwakua kuna baadhi ya mamlaka za Serikali za Mitaa zinaripotiwa kuwaonea
sana wananchi hasa wanawake katika kupata haki zao maana ndio
wanaongoza kwa kunyanyaswa.
Pia amewataka Wakuu wa Mikoa
kutumia mamlaka waliyopewa kuvunja mabaraza yote ya usuluhishi
yasiyozingatia sheria katika kutoa maamuzi na kuunda mabaraza mapya
yenye sifa za kutatua kesi za wananchi.
Naye Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya
Rais,TAMISEMI, Mhe. Selemani Jaffo ameahidi kuwapa Wakuu wa Mikoa
ushirikiano wa kutosha kutoka Ofisi ya TAMISEMI ili kuhakikisha kazi zao
zinafanyika kwa ufanisi.
No comments:
Post a Comment