Rais
wa Vietnam Mhe. Truong Tang Sang akiwa pamoja na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia
wananchi na wafanyakazi wa Ikulu mara baada ya kuwasili.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akifurahia jambo na Rais wa Vietnam Mhe. Truong Tang Sang wakati
walipokuwa wanazungumza Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akiongoza Mazungumzo Rasmi kati ya ujumbe wa Tanzania na Ujumbe wa Rais
wa Vietnam Mhe. Truong Tang Sang Ikulu jijini Dar es Salaam
Rais
wa Vietnam Mhe. Truong Tang Sang akimshukuru Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya
kuzungumza na wanahabari hawapo pichani Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akizungumza na wanahabari hawapo pichani kuhusu mazungumzo yao na Rais
wa Vietnam Mhe. Truong Tang Sang Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akimsindikiza mgeni wake Rais wa Vietnam Mhe. Truong Tang Sang Ikulu
jijini Dar es Salaam.
PICHA NA IKULU
WAZIRI MKUU: TANZANIA YAPIGA HATUA KIUCHUMI
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amesema mabadiliko ya kiuchumi yaliyofanyika
nchini yameifanya Tanzania ipige hatua kubwa katika kipindi cha miaka 10
iliyopita.
"Kumekuwa
na mabadiliko chanya kwenye ukuaji halisi wa Pato la Taifa, kushuka kwa
mfumuko wa bei, na akiba ya kutosha ya fedha za kigeni. Pato la Taifa
limekua kwa wastani wa asilimia 7 na mfumuko wa bei umeshuka hadi
kufikia asilimia 5.3 mnamo Juni 2015 ikilinganishwa na asilimia 16 na
asilimia 8 ilivyokuwa mwishoni mwa mwaka 2012 na mwanzoni wa mwaka
2013," alisema.
Ametoa
kauli hiyo leo jioni (Jumatano, Machi 9, 2016) wakati akihutubia
kongamano la biashara baina ya Tanzania na Vietnam lililofanyika kwenye
ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam na
kuhudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Kisoshalisti ya Vietnam, Bw. Troung Tan Sang.
Akizungumza
kwa niaba ya Rais, Dk. John Pombe Magufuli, Waziri Mkuu alisema mbali
ya mabadiliko ya kiuchumi, Tanzania pia imefanya mabadiliko kwenye
sheria, mifumo ya kifedha na sekta za kuhudumia jamii za umma.
"Katika
kipindi cha muongo mmoja uliopita tumefanya mabadiliko ya kisera na
kwenye sheria zetu ili kuboresha hali ya uwekezaji, kukuza uchumi na
kuboresha maisha ya wananchi," alisema.
Alitoa
mwaliko kwa wafanyabiashara walioambatana na Rais wa nchi hiyo kwa
kuwaeleza kwamba faida kubwa ya kuwekeza nchini Tanzania ni uwepo wa
soko la uhakika kwa wakazi zaidi ya milioni 300 waishio Mashariki na
Kusini mwa bara la Afrika.
"Tanzania
ni mwanachama wa Jumuiya za Kikanda katika SADC na EAC. Uwepo wake
katika taasisi hizi ni fursa tosha. Pia Tanzania ni lango kwa nchi sita
ambazo hazipakani na bahari. Inasaidia kufanyika biashara katika nchi za
Congo (DRC), Rwanda, Burundi, Zambia, Malawi na Uganda," alisema.
Akizungumzia
kuhusu fursa zilizopo kwenye sekta ya kilimo, Waziri Mkuu
aliwakaribisha wafanyabiashara hao wawekeze kwenye kilimo cha biashara
na viwanda vya usindikaji ili waweze kusaidia kuongeza uzalishaji wa
chakula nchini.
"Tuwakaribisha
kuwekeza kwenye viwanda vya usindikaji ili kuongeza thamani za mazao
yanayozalishwa nchini, kujenga viwanda vidogo vya kutengeneza
vifungashio kwa ajili ya masoko ya ndani na nje ya nchi. Pia mnaweza
kuwekeza kwenye utengenezaji wa zana za kilimo ambazo ni za bei nafuu
kwa wananchi wetu," alisema.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S. L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM.
JUMATANO, MACHI 9, 2016.
WAZIRI MWAKYEMBE AMTEMBELEWA NA BALOZI WA SWEDEN.
Waziri
wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Harisson Mwakyembe akiongea na Balozi wa
Sweden (mwenye suti nyekundu) alipomtembelea ofisini kwake kwa ajili ya
kubadilishana mawazo kuhusu sekta ya sheria leo (9/3/2016) jijini Dar Es
Salaam. Mwenye suti ya bluu upande wa kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa
Wizara ya Katiba na Sheria Ndg. Amon mpanju.
Balozi
wa Sweden nchini Tanzania Bi. Katarina Rangnitt akisisitiza jambo
wakati akiongea na Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Harisson Mwakyembe
alipomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam.
MAMA JANETH MAGUFULI AMKARIBISHA MKE WA RAIS WA VIETNAM, BI. MAI THI HANH OFISINI KWAKE.
Mke
wa Rais wa Vietnam, Bi. Mai Thi Hanh (mwenye gauni jekundu)
akisalimiana na akina mama waliompokea mara alipotembelea katika ofisi
za mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Janeth Magufuli 9
Machi, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Mke
wa Rais wa Vietnam, Bi. Mai Thi Hanh (mwenye gauni jekundu)
akisalimiana na wacheza ngoma mara alipotembelea katika ofisi za mke wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Janeth Magufuli 9 Machi,
Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Mke
wa Rais wa Vietnam, Bi. Mai Thi Hanh akisaini kitabu cha wageni mara
alipowasili katika ofisi za mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mama Janeth Magufuli (kulia) 9 Machi, Ikulu Jijini Dar es
Salaam.
Mke
wa Rais wa Vietnam, Bi. Mai Thi Hanh (kushoto) akifurahia zawadi ya
kinyago cha kuchonga alichokabidhiwa na mwenyeji wake mama Janeth
Magufuli kama zawadi 9 Machi, 2016 katika ofisi za Mke wa Rais Jijini
Dar es Salaam.
Mke
wa Rais wa Vietnam, Bi. Mai Thi Hanh (kushoto) akimpa zawadi mama
Janeth Magufuli ikiwa shukurani yake mara alipotembelea katika ofisi
yake 9 Machi, 2016 Jijini Dar es Salaam.(PICHA ZOTE NA BENEDICT
LIWENGA-MAELEZO).
No comments:
Post a Comment