MKUU WA WILAYA YA WANGING'OMBE DKT ASUNTA MSHANA AKIHUBIRI KATIKA KANISA LA EAGT NJOMBE CHAUGING
WAUMINI WAKIOMBA NA KUNENA KWA LUGHA KATIKA KIANISA LA EAGT LILILOPO CHAUGINGI NJOMBE MJINI
MZEE WA KANISA NASISI VENANCE AKITOA MAELEKEZO KWA WAUMINI JUU YA ULINZI WA WATOTO WADOGO WAKATI WAKIWA KANISANI
HAPA MKUU HUYO WA WILAYA ASUNTA MSHANA YUPO KUTOA NENO LA KIROHO KWA WAUMINI WA KANISA HILO
KWAYA YA KANISA LA EAGT IKIBURUDISHA KWA KUIMBA NYIMBO ZAO ZA KUSIFU JINA LA MUNGU KANISANI HAPO
MZEE HUYUY AMBAYE NI MUUMINI WA KANISA HILO ANAKWENDA KUMSHIKA MKONO BAADA YA KUGUSWA NA NENO LINALOTOLEWA KANISANI HAPO
Mkuu Wa Wilaya Ya Wanging'ombe Mkoani Njombe Asunta Mshana Amewataka Wananchi Kuziacha Imani Potofu Za Mfumo Dume Unaofanywa Na Baadhi Ya Jamii Katika Familia Yakwamba Mwanamke Hastahili Kupata Urithi Wa Mali Baada Ya Wazazi Wake Kufariki Kwa Madai Anayestahili Ni Kijana Wa Kiume.
Akizungumza Mara Baada Ya Kumaliza Ibada Katika Kanisa La Evanjelistic Assembles Of God Tanzania Lililopo Chaugingi Mjini Njombe Mkuu Wa Wilaya Ya Wanging'ombe Dkt Asunta Mshana Amesema Mfume Dume Kwa Sasa Hauna Nafasi Huku Akitaka Wakristo Kukemea Baadhi Ya Watu Wanaoendekeza Mfumo Huo Kandamizi Kwa Wanawake.
Aidha Dkt Mshana Amesema Serikali Inakwenda Kutunga Katiba Mpya Itakayokuwa Na Vifungu Vya Kuwalinda Wanawake Nakwamba Kila Mmoja Anatakiwa Kupata Haki Sawa Katika Kurithi Mali Kwani Binadamu Wote Ni Sawa Na Hivyo Kila Mmoja Kwenye Familia Anapaswa Kupewa Haki Yake.
Aidha Mkuu Huyo Wa Wilaya Dkt .Mshana Amekemea Pia Tabia Ya Kuwatumikisha Kazi Za Ndani Watoto Wa Kike Bila Kuwapatia Ujira Unaostahili Ambapo Amesema Biblia Inasema Vibarua ,Watumishi Wa Kazi Za Ndani Wote Watakuwepo Lakini Wanatakiwa Kuthaminiwa Kama Watu Wengine.
asante sana
ReplyDelete