Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Monday, March 7, 2016

MKUU WA WILAYA YA WANGING'OMBE DKT ASUNTA MSHANA AKEMEA UWEPO WA MFUMO DUME UNAOFANYWA NA WANAUME


 

 MKUU  WA WILAYA YA WANGING'OMBE DKT ASUNTA MSHANA AKIHUBIRI KATIKA KANISA LA EAGT  NJOMBE CHAUGING
 WAUMINI WAKIOMBA NA KUNENA KWA LUGHA KATIKA KIANISA LA EAGT LILILOPO CHAUGINGI NJOMBE MJINI


 MZEE WA KANISA  NASISI VENANCE  AKITOA MAELEKEZO KWA WAUMINI  JUU YA ULINZI WA WATOTO WADOGO  WAKATI WAKIWA KANISANI


 HAPA MKUU HUYO WA WILAYA  ASUNTA MSHANA YUPO KUTOA NENO LA KIROHO KWA WAUMINI WA KANISA HILO










 KWAYA YA KANISA LA EAGT IKIBURUDISHA KWA KUIMBA NYIMBO ZAO ZA KUSIFU JINA LA MUNGU KANISANI HAPO



 MZEE HUYUY AMBAYE NI MUUMINI WA KANISA HILO ANAKWENDA KUMSHIKA MKONO BAADA YA KUGUSWA NA NENO LINALOTOLEWA KANISANI HAPO







Mkuu Wa Wilaya Ya Wanging'ombe  Mkoani Njombe Asunta Mshana Amewataka Wananchi Kuziacha Imani Potofu Za Mfumo Dume Unaofanywa Na Baadhi Ya  Jamii Katika Familia Yakwamba Mwanamke Hastahili Kupata Urithi Wa Mali  Baada Ya Wazazi Wake Kufariki Kwa Madai Anayestahili Ni Kijana Wa Kiume.

Akizungumza  Mara Baada Ya Kumaliza Ibada Katika  Kanisa La Evanjelistic   Assembles Of God   Tanzania Lililopo  Chaugingi  Mjini Njombe  Mkuu Wa Wilaya Ya  Wanging'ombe Dkt Asunta Mshana Amesema  Mfume Dume Kwa Sasa Hauna Nafasi  Huku Akitaka Wakristo Kukemea  Baadhi Ya  Watu Wanaoendekeza Mfumo Huo  Kandamizi Kwa Wanawake.

Aidha Dkt Mshana Amesema  Serikali Inakwenda Kutunga Katiba Mpya  Itakayokuwa Na Vifungu Vya Kuwalinda Wanawake  Nakwamba Kila Mmoja Anatakiwa Kupata Haki Sawa Katika Kurithi Mali  Kwani Binadamu Wote Ni Sawa   Na Hivyo Kila Mmoja  Kwenye Familia Anapaswa Kupewa Haki Yake.

Aidha Mkuu Huyo Wa Wilaya Dkt .Mshana  Amekemea Pia Tabia Ya Kuwatumikisha  Kazi Za Ndani  Watoto Wa Kike  Bila Kuwapatia Ujira Unaostahili  Ambapo Amesema Biblia Inasema  Vibarua ,Watumishi Wa  Kazi Za Ndani  Wote Watakuwepo Lakini  Wanatakiwa  Kuthaminiwa  Kama Watu Wengine.

1 comment: