MKUU WA MKOA AKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA , EMELDA SALUM NI MHANDIS WA TCRA MAKAO MAKUU DAR ES SALAAM WA UPANDE WA KULIA,, WAPILI KUTOKA KULIA NI MKUU WA WILAYA YA NJOMBE BI.SARAH DUMBA, WA TATU KUTOKA KULIA NI MKUU WA MKOA WA NJOMBE DKT REHEMA NCHIMBI NA WA NNE KUTOKA KULIA NI LILIAN MWANGOKA MENEJA WA MAMLAKA YA MAWASILIANO NYANDA ZA JUU KUSINI .
AWALI AKITOA HOTUBA KWA WADAU WA MAWASILIANO MKUU WA MKOA WA NJOMBE DKT REHEMA NCHIMBI AKIWA KATIKA UKUMBI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA NJOMBE
MKUU WA MKOA WA NJOMBE MGENI RASMI KWENYE MAFUNZO YA MAWASILIANO AKIWASILI KATIKA UKUMBI WA SEMINA KATIKA UKUMBI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA NJOMBE.
KAMATI YA ULINZI NA USALAMA YA MKOA WA NJOMBE
MKUU WA WILAYA YA NJOMBE BI.SARAH DUMBA AKIMKARIBISHA MKUU WA MKOA WA NJOME AWEZE KUZUNGUMZA NA WADAU
WADAU WA MAWASILIANO AMBAO NI WAFANYABIASHARA WA SIMU ZA MKONONI
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Imetoa Mafunzo Kwa Wafanyabiashara wa Simu za Mkononi Pamoja na Wadau wa Mawasiliano Jinsi ya Kuzitambua Simu Bandia
Mafunzo Hayo Yametolewa Kwa Wadau wa Mawasiliano Huku Idadi Kubwa ya Wananchi Wakitumia Simu Zisizo na Ubora Huku TCRA Ikitangaza Kuzizima Simu Ambazo Hazina Viwango Vya Ubaora wa Kimataifa Ifikapo Juni 17 Mwaka Huu na Kwamba Tayari Wananchi Wanatumia Ujumbe Kuhusiana na Simu Zao
Akizungumza na Waandishi wa Habari Pembeni Mwa Mafunzo Hayo Meneja wa TCRA Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Lilian Mwangoka Amesema Lengo la Serikali ni Kudhibiti Simu Zisizo na Ubora Kuingia Nchi Pamoja na Athari Zitokanazo na Simu Hizo.
Awali Akifungua Mafunzo Hayo Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dkt. Rehema Nchimbi Ambaye Alikuwa Mgeni Rasmi Amewataka Wananchi Kutumia Mawasiliano Katika Kukuza Uchumi na Maendeleo Hukua Akiwataka Wafanyabiashara wa Simu Kuacha Kuuza Simu Zisizo na Ubora.
Kwa Upande Wao Baadhi ya Washiriki wa Mafunzo Hayo Hasa Wafanyabiashara wa Simu Akiwemo Eliyud Fabiani Pangamawe Wameomba Serikali Kuongeza Kasi ya Utoaji Elimu Kwa Wananchi na Wafanyabiashara Namna ya Kizitambua Simu Zisizo na Ubora
Wamesema Kwa Sasa Wataanza Kuingiwa Hasara Ya Simu Kwani Tayari Mzigo Wa Simu walikwisha kununua huku wakisema elimu hiyo imetolewa na imepokelewa vizuri lakini hawajaoneshwa wakanunuwe wapi kwenye simu zisizofeki.
No comments:
Post a Comment