MKUU wa
Mkoa wa Dar es Salaam ameanza kazi rasmi leo mchana ambapo alifanya
mazungumzo na wakuu wa idara na Vitengo mbalimbali na kutoa maagizo
mazito ambapo alitoa masaa 24 kwa wakuu hao ya kumpa taarifa zilizopo
katika maeneo yao husika zenye kuelezea changamoto mbalimbali ili kuona
wananchi wanakabiliwa na changamoto zipi na namna atakavyoweza
kuzitatua.
Makonda
aliyasema hayo wakati akizungumza na wakuu hao wa idara na vitengo
katika hafla fupi ya kukaribishwa kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi ya
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ambapo mbali ya wakuu hao wa idara na
vitengo pia ilihudhuriwa na Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi na Makatibu
Tawala wa wilaya zote za mkoa wa Dar es Salaam.
Awali
Makonda alimshukuru Mwenyezi Mungu kwa kufanikisha yeye kushika nafasi
hiyo baada ya Mheshiwa Rais Dk.John Magufuli kusikia sauti ya Mungu na
kuifanyia kazi ya kumchagua kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Aidha
Makonda alimshukuru Rais Dk.John Magufuli kwa kumuamini na kumteua
kushika nyazifa hiyo muhimu ya kuwatumikia wananchi ambapo pia
alimshukuru Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam wa zamani, Saidi Meck Sadiki kwa
kumpokea akiwa kama Mkuu wa Wilaya na kumfundisha mambo mengi makubwa na
mazuri ambayo yamemfanya kwa namna moja au nyingine kupata nafasi hiyo
ya ukuu wa mkoa.
Makonda
amesema kwamba kwa sasa hajui chochote badala yake amewaomba watendaji
wote kuonesha ushirikiano kati yao ili kuupeleka kwa kasi mkoa wa Dar es
Salaam kimaendeleo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (katikati), akizungumza na wakuu wa idara mbalimbali katika ofisi yake.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akishukua kutoka kwenye gari lake
la Ukuu wa Mkoa wakati alipokuwa akifika kwa mara ya kwanza ofisini
kwake Dar es Salaam leo mchana.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (katikati), akizungumza na wakuu wa idara mbalimbali katika ofisi yake.
Mkuu
wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema, akimkabidhi kadi ya kumkaribisha
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya
Ilala, Raymond Mushi.
Katibu
Tawala Msaidizi- Utawala, Ellha Mcha (kushoto), akisalimiana na Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda baada ya kumpokea rasmi jana
alipofika kwa mara ya kwanza katika ofisi yake.
Mhasibu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Shabani Mhando akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
Mkurugenzi mpya wa Manispaa ya Kinondoni, Aron Kagurumjuli akisalimiana na Mkuu mpya wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
Katibu
Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mmbando (kushoto),
akizungumza wakati wa kumakribisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul
Makonda. Kutoka kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema, Mkuu wa
Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi na RC Paul Makonda.
Wakuu wa Idara mbalimbali katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam wakiwa kwenye hafla ya kumpokea mkuu wao wa mkoa.
Mkutano ukiendelea.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema (kulia), akizungumza wakati akimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
Na Dotto Mwaibale
No comments:
Post a Comment