MWENYEKITI WA KIJIJI CHA IGORA KATA YA LUPONDE AKIWAONESHA ENEO LA ZAHANATI YA MTAA WA IDUCHU MBUNGE EDWARD MWALONGO AKIWA NA DIWANI WA KATA HIYO ULRICK MSEMWA PAMOJA NA AFISA TARAFA YA IGOMINYI
WANANCHI WA MTAA WA IDUCHU WAKIWA KWENYE MKUTANO WA HADHARA WA MBUNGE NA DIWANI LUPONDE
WAZEE WA KIJIJI CHA IGORA WAKIWA KWENYE MKUTANO HUO
DIWANI WA KATA YA LUPONDE ULRICK MSEMWA AKIZUNGUMZA NA WANANCHI
MBUNGE WA JIMBO LA NJOMBE MJINI EDWARD MWALONGO AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WA MTAA WA IDUCHU WAKIWA KATIKA ZAHANATI YA MTAA HUO.
WANANCHI WA IDUCHU WAMESEMA WANYAMA WAHARIBIFU WANAWASUMBUA KWA KUMALIZA MAZAO YAO YA MAHINDI
MWENYEKITI WA KIJIJI CHA IGORA JOHN MWAPINGA AKIZUNGUMZA MBELE YA MBUNGE
HILI NI BWENI LA WASICHANA KATIKA SHULE YA MSINGI LUHOLOLO
Mbunge Wa Jimbo La Njombe Kusini Edward Mwalongo Ameahidi Kupeleka Mifuko 20 Ya Saruji Na Makopo Matano Ya Rangi Katika Kijiji Cha Igola Kata Ya Luponde Vyenye Thamani Ya Shilingi Laki Tatu Huku Akipongeza Kwa Jitihada Wanazofanya Wananchi Za Ujenzi Wa Miundombinu Ya Zahanati Na Madarasa Ya Shule.
Akizungumza Kwenye Mkutano Wa Kuwashukuru Wananchi Kwa Kumchagua Mbunge Edward Mwalongo Ametaka Wadau Kuchangia Ujenzi Wa Mradi Wa Zahanati Na Kutaka Waache Kuendekeza Siasa Badala Yake Wafanye Kazi Ili Mradi Huo Ukamilike Kwa Wakati Huku Akiwaomba Viongozi Kusimamia Kwa Umakini Asiwepo Wakuiba Vifaa Vya Zahanati Hiyo.
Aidha Mwalongo Amesema Tatizo La Umeme Bado Wanaendelea Kulifanyia Kazi Kadri Serikali Ilivyoahidi Ambapo Amesema Ifikapo Mwezi Decemba Mwaka Huu Wananchi Wa Vijiji Mbalimbali Vya Halmashauri Ya Mji Vitakuwa Na Umeme Vikiwemo Vijiji Vya
Luhololo,Igora ,Iwungilo Na Vijiji Vingine Vya Halmashauri Ya Mji Wa Njombe.
Kwa Upande Wake Diwani Wa Kata Ya Luponde Ulrick Msemwa Amesema Pamoja Na Mafanikio Yanayopatikana Kwenye Kata Hiyo Lakini Bado Wanakabiliwa Na Ukosefu Wa Nyumba Za Walimu Ambapo Kwa Sasa Wanaendelea Na Ujenzi Wa Bweni La Sichana Katika Shule Ya Sekondari Luhololo ,Na Uwepo Wa Tatizo La Uharibifu Wa Miundombinu Ya Barabara.
Akisoma Taarifa Fupi Mbele Ya Mbunge Huyo Afisa Mtendaji Wa Kijiji Cha Igola Pradusi Mwapinga Amesema Kijiji Hicho Kimefanikiwa Kusimamia Ujenzi Wa Madarasa Mawili Ya Chekechea Darasa Moja Mtaa Wa Njirikwa Na Mtaa Iduchu, Kuendelea Na Utekelezaji Wa Zahanati Katika Mitaa Yote Miwili Huku Changamoto Ikiwa Ni Kukosa Madawati,Mifuko Ya Saruji,Kukosekana Kwa Mganga Na Maji Katika Mtaa Wa Iduchu.
No comments:
Post a Comment