Mwalimu Mkuu Shule Ya Msingi Igora Godlove Myungile Akizungumza Na Mbunge Mwalongo Ofisini Kwake Kuhusiana Na Fedha Za Keptesheni Haziwafikia Tangu Mwezi Januari Hadi Mwezi Huu.
WANAFUNZI DARASA LA AWALI IGORA
MBUNGE MWALONGO AKIWAKABIDHI KALAMU WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI IGORA AKIWA NA AFISA TARAFA WA IGOMINYI MWENYE MIWANI
MBUNGE WA JIMBO LA NJOMBE MJINI EDWARD MWALONGO ANAKABIDHI KALAMU NA DAFTARI KWA WANAFUNZI KATIKA SHULE YA MSINGI IGORA
MBUNGE WA JIMBO LA NJOMBE MJINI EDWARD FRANZ MWALONGO AKIWA SHULE YA MSINGI IGORA KUKABIDHI MSAADA WA MAHITAJI YA SHULE KWA WANAFUNZI WA DARASA LA KWANZA NA LA SABA.
Mbunge Wa Jimbo La Njombe Kusini Amemtaka Afisa Elimu Shule Za Msingi Halmashauri Ya Mji Wa Njombe Kupeleka Walimu Wa Katika Shule Zilizokosa Walimu Wa Kike Ili Kuweka Usawa Kwa Wanafunzi Huku Akiahidi Kufuatilia Fedha Za Captasheni Katika Shule Ya Msingi Igola Ambayo Haijafanikiwa Kupata Tangu Januari Hadi Mwezi Huu.
Akizungumza Wakati Akikabidha Msaada Wa Mahitaji Ya Shule Kwa Wanafunzi Na Walimu Wa Shule Ya Msingi Igola Ikiwemo Daftari,Chaki Na Kalamu Kwa Madarasa Ya Darasa La Kwanza Na La Saba Mbunge Wa Jimbo La Njombe Kusini Edward Mwalongo Amewahimiza Wanafunzi Hao Kusoma Kwa Bidii Kwa Manufaa Yao Ya Baadaye .
Aidha Mwalongo Amekemea Tabia Ya Utoro Kwa Wanafunzi Wa Shule Za Msingi Katika Jimbo Hilo Na Kutaka Wazazi Kushirikiana Na Walimu Kudhibiti Tabia Ya Utoro Shuleni Huku Akipongeza Jitihada Za Ujenzi Wa Darasa La Chekechea Linalojengwa Katika Shule Ya Msingi Igola .
Kwa Upande Wake Mwalimu Mkuu Wa Shule Ya Msingi Igola Godlove Myungile Amesema Shule Hiyo Inakabiliwa Na Changamoto Ya Kukosekana Kwa Fedha Ya Captesheni Tangu Januri , Ukosefu Wa Walimu Wa Jinsi Ya Kike Ambapo Walimu Waliopo Ni sita Nao Ni Wakiume Pekee Jambo Ambalo Linasababisha Kukosekana Kwa Usawa Na Uhuru Wa Kueleza Matatizo Ya Watoto Wa Kike Shuleni.
Diwani Wa Kata Ya Luponde Ulrick Msemwa Ameshukuru Kwa Msaada Uliotolewa Na Mbunge Huyo Wa Kusaidia Vifaa Kwa Wanafunzi Wa Shule Ya Msingi Igora Na Kusema Kuwa Kijiji Hicho Kinakabiliwa Na Changamoto Ya Ujenzi Wa Darasa La Chekechea Na Zahanati Ya Kijiji Cha Igora Ambayo Ipo Kwenye Hatua Ya Msingi Inayojengwa Kwa Ushirikiano Wa Shirika La Shikujanjo.
No comments:
Post a Comment