Mbunge wa Busega na Kaimu
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Maendeleo ya jamii
Mh. Raphael Chegeni akisaini kitabu cha wageni mara baada ya wajumbe wa
kamati hiyo kuwasili katika ofisi za Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa
jijini Dar es salaam ambapo kamati hiyo imekutana na uongozi wa mfuko
huo ili kusikiliza mipango yao ya baadae na changamoto mbalimbali
zinazoikabili taasisi hiyo ikiwa ni pamoja na mafanikio na kuangalia
mambo kadhaa yanayokwamisha shughuli za mfuko huo ili hatua za
kurekebisha zichukuliwe na kwa ajili ya kufanya mfuko huo kusaidia
jamii katika suala zima la afya , Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa mfuko
huo Bw. Michael Muhando.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
Mbunge wa Busega na Kaimu
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Maendeleo ya jamii
Mh. Raphael Chegeni akisaini kitabu cha wageni na mbunge wa Kigoma mjini
Mh. Zitto Kabwe wakati wajumbe wa kamati hiyo walipowasili katika ofisi
za mfuko huo Kurasini jijini Dar es salaam.
Mbunge wa Busega na Kaimu
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Maendeleo ya jamii
Mh. Raphael Chegeni pamoja na wajumbe wa kamati hiyo wakiendelea na
utaratibu wa kusaini kitabu cha wageni.
Wajumbe wa Kamati ya kudumu ya
Bunge ya Maendeleo ya Jamii wakielekea mwenye ukumbi wa mkutano kwa
ajili ya kupewa taarifa na Kaimu Mkurugenzi wa mfuko huo Bw. Michael
Muhando wa kwanza kulia.
Kutoka kulia ni Mbunge wa Ilala
Mh. Azzan Zungu, Mbunge wa Kigoma Mh. Zitto Kabwe, Kaimu Mwenyekiti wa
kamati hiyo na Mbunge wa jimbo la Busega Dk. Raphael Chegeni, Mbunge wa
Kigamboni Mh. Dk. Faustine Ndugulile, Kaimu Mkurugenzi wa Mfuko wa Bima
ya afya NHIF Bw. Michael Muhando na Mkurugenzi wa huduma za utabibu na
ufundi Dk.Frank Lekey wakielekea kwenye mkutano.
Mbunge wa Busega na Kaimu
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Maendeleo ya jamii
Mh. Raphael Chegeni akizungumza katika mkutano huo huku Naibu Waziri wa
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi
Kigwangalla (katikati) akifuatilia mkutano huo, kulia ni mjumbe wa
kamati hiyo Mbunge wa Kigamboni Mh. Dk. Faustine Ndungulile.
Wajumbe wa kamati hiyo
wakisikiliza wakati Kaimu Mkurugenzi wa NHIF alipokuwa akiwasilisha
ripoti ya shirika hilo kwa kamati hiyo leo.
Baadhi ya wakurugenzi wa vitengo
NHIF wakifuatilia mambo kadhaa wakati wa uwasilishaji wa ripoti hiyo
mbele ya Makamti ya Bunge Maendeleo ya Jamii, kutoka kulia ni
Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa NHIF, Rehani Athumani na Ali Othman
Mkurugenzi wa TEHAMA NHIF.
Mjumbe wa kamati Mbunge wa Buchosa Mh. Dk Charles Tizema akitoa mchango wake katika mkutano huo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akifafanua
jambo mbele ya kamati hiyo wakati wa mkutano huo kutoka kushoto ni Kaimu
Mkurugenzi wa NHIF Bw. Michael Mhando na katikati ni Kaimu Mwenyekiti
wa Kamati na Mbunge wa jimbo la Buseka Dk. Raphael Chegeni.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk . Mpoki Ulisubisya
akifafanua jambo mbele ya kamati hiyo huku wabunge wakifuatilia.
Kaimu Mkurugenzi wa NHIF Bw.
Michael Mhando akitoa ufafanuzi wa mambo kadhaa yaliyojadiliwa na kamati
hiyo pamoja na uongozi wa NHIF.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akikagua
kituo cha huduma kwa wateja kwa njia ya simu kilichoanzishwa kwa ajili
ya kuwafanya wateja kupata taarifa mbalimbali kuhusu mfuko huo bila
kulazimika kufika ofisini.
Katibu Mkuu wa Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Mpoki Ulisubisya
akiongozwa na Kaimu Mkurugenzi wa NHIF Bw. Michael Muhando wakati
akielekea kukagua eneo linaohifadhi kumbukumbu za mfuko huo.
No comments:
Post a Comment