Mkuu wa Wilaya ya Wanging'ombe Dokta Asumpta Mshama Akizungumza na Wakazi wa Kijiji Cha Mhaji Kabla ya mkutano Kuvunjika
Askari Polisi Wakimpa Ulinzi DC Baada ya Kuingia Kwenye Gari Baada ya Mkutano Kuvurugika Kijijini Mhaji
Na Gabriel Kilamlya WANGING'OMBE
Katika Hali Isiyo ya Kawaida Mkuu wa Wilaya ya Wanging'ombe Mkoani Njombe Dokta Asumpta Mshama Amejikuta Katika Wakati Mgumu Wakati Akizungumza na Wananchi wa Kijiji Cha Mhaji Kufuatia Tukio La Askari Polisi Kudaiwa Kufika Kijijini Hapo Usiku wa Kuamkia Machi 10 Mwaka Huu na Kuwakamata Watu Watano Ambao ni Ndugu na Kuwapeleka Kituoni Kwa Madai ya Kumtishia Mzee Mmoja Kuwa Anajihusisha na Imani za Kishirikina.
Ni Mwenyekiti wa Kijiji Cha Mhaji Obeid Salingwa Ambaye Alikuwa Akijaribu Kuwatuliza Wananchi Wake Ambao Wameonekana Kuwa na Jazba Baada ya Mkuu wa Wilaya ya Wanging'ombe Kukataa Kuwahusisha Askari Polisi na Vitendo Vya Uvutaji Bangi.
Hatua Hiyo Imekuja Baada ya Hotuba Ndefu ya Mkuu Huyo wa Wilaya Iliyolenga Kumaliza Mgogoro Huo na Ilipofikia Hatua ya Kuanza Kuwatetea Askari Wanaodaiwa Kudiriki Kuvuta Bangi Kwenye Nyumba ya Mtuhumiwa Mmoja Wapo Wakati wa Tukio la Kuwakamata Watu Hao Wanaosadikaki Kumtishia Mzee Huyo.
Akizungumza Kijijini Hapo Dokta Mshama Ambaye Alianza Kwa Kukemea Tabia za Kutuhumiana Uchawi Hadi Karne Hii Amesema Pamoja na Tuhuma Hizo Lakini Hakunabudi Kuwahoji Watuhumiwa Hao Watano Waliokamatwa na Jeshi la Polisi Ili Kuelezea Vitendo Vya Kishirikina Wanavyovieleza.
Ndugu Hao Watano Ukoo wa Akina Wandelage Walikwenda Kuwekewa Dhamana na Kundi la Wananchi Baada ya Kukamatwa Usiku Huo na Kwamba Baba Yao Alionekana Kulikwepa Jambo Hilo Ilihali Wanaona Wenzao Watatu Wanaendelea Kuumwa Bila Kufahamu Kinachowasumbua Pamoja na Kupelekwa Kwenye Hospitali Mbalimbali.
Katika Mkutano Huo Wananchi Wakapewa Fursa ya Kuuliza Maswali Ambapo Hoja Kubwa Ililenga Vurugu Zilizofanywa na Askari Polisi Wanaodaiwa Kwenda Usiku Huo na
Kuwaletea Vurugu Wananchi Hao Watano na Mwingine Kumjeruhi.
Hata Hivyo Sababu Kubwa ya Kuvunjika Kwa Mkutano Huo Ilianzia Pale Ambapo Baadhi ya Wananchi Walipoanza Kuwatuhumu Askari Waliofika Usiku Huo Kuwa Walikuwa Wakivuta Bangi Jambo Ambalo Mkuu Huyo wa Wilaya Ameonekana Kutokubaliana Nalo.
Licha ya Dhoruba Hiyo Lakini Mkuu Huyo wa Wilaya Alifika Kijijini Hapo Kwa Lengo la Kutaka Kutatua Mgogoro wa Mipaka na Kukutana na Sakata Hilo.
No comments:
Post a Comment