Katibu
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Thomas
Kashililah (kulia) akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Bunge la Israel
wakati alipomtembelea leo ofisini kwake Jijini Dar es Salaam na kufanya
mazungumzo naye.
Katibu
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Thomas
Kashililah (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa
Bunge la Israel, Rone Plotwakati alipomtembelea leo ofisini kwake jijini
Dar es Salaam na kufanya mazungumzo naye.
Katibu
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Thomas
Kashililah (kulia) akiongea na Mkurugenzi Mkuu wa Bunge la Israel, Rone
Plot wakati wa chakula cha mchana katika hoteli ya Kilimanjaro iliyopo
jijini Dar es Salaam.
Katibu
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Thomas
Kashililah (kulia) akimkabidhi zawadi ya trei ya kubebea vinywaji mke wa
Mkurugenzi Mkuu wa Bunge la Israel, Bi. Shosh Plot wakati wa chakula
cha mchana katika hoteli ya Kilimanjaro iliyopo jijini Dar es Salaam.
Katibu
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Thomas
Kashililah (kulia) akipokea zawadi toka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Bunge la
Israel, Ronen Plot wakati wa chakula cha mchana katika hoteli ya
Kilimanjaro iliyopo jijini Dar es Salaam.
Katibu
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Thomas
Kashililah (wa pili kulia)akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi
Mkuu wa Bunge la Israel, Ronen Plot (wa pili kushoto) wakati wa chakula
cha mchana katika hoteli ya Kilimanjaro iliyopo jijini Dar es Salaam.
Kushoto ni Naibu Katibu wa Bunge John Joel
Na Zuhura Mtatifikolo, Bunge
Katibu wa Bunge Tanzania Dkt
Thomas Kashililah leo amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu
wa Bunge la Israeli (KNESSET) Ronen Plot aliyemtembelea Ofisini kwake
jijini Dar es Salaam akitokea Nchini Zambia alikokuwa akishiliki Mkutano
wa 134 wa umoja wa Mabunge Duniani (IPU) uliofanyika tarehe 19 hadi 23
Machi, 2016.
Akizungumzo wakati wa kikao na
Dkt. Kashililah, Mkurugenzi huyo wa Bunge la Israel, amesema ziara yake
hapa nchini kutembelea Bunge la Tanzania ina lengo la kuwasilisha
Mkataba wa Makubaliano wenye lengo la kuanzisha cha Urafiki wa Kibunge
baina ya Bunge la Tanzania na Bunge la Israel.
Plot ambaye alimbatana na mkewe
Shosh Plot, amesema Bunge la Israel linautaratibu wa kuwa na mahusiano
na mabunge mengine duniani kwa lengo la kubadilishana uzoefu katika
masuala ya uendeshaji Mabunge ambapo hadi kufikia sasa tayari Bunge hilo
lina ushirikiano wa karibu kupitia utaratibuy huu na mabunge zaidi ya
30 Duniani kote na kwa upande wa Afrika ni nchi Tano walizotiliana
saiani na kuanzisha ushirikiano wa namna hiyo.
Akielezea, nia hiyo ya Bunge la
Israel, Katibu wa Bunge la Tanzania Dkt Thomas Kashililah amesema
amefurahishwa sana na ujio wa Mkurugenzi wa Bunge hilo kutembelea Bunge
la Tanzania na tayari wamezingatia kwenye mipango uanzishwaji wa Chama
cha Ushirikiano wa Mabunge haya mawili kikihusisha Wabunge kutoka pande
zote mbili kubadilishana mawazo hususani katika namna bora ya uendeshaji
na usimamizi wa shughuli za kibunge.
Katika kufanikisha hilo, Dkt.
Kashililah amesema ujumbe huo utakutana na Spika wa Bunge Mhe. Job
Ndugai siku ya Jumamosi ili kufanya mazungumzo nae na kisha kuangalia
namna utekelezaji wa wazo hilo utakavyokuwa kabla ya kutiliana saiani
makubaliano hayo.
Tayari Bunge la Tanzania lina
makubaliano ya ushirikiano na vyama vya kirafiki kutoka Mabunge mengine
ya Nchi mbalimbali duniani ambazo ni Uturuki, China, Korea Kusini,
Morroco, Misri, Uholanzi na Poland

No comments:
Post a Comment