● Aziagiza Halmashauri kushughulikia migogoro ya ardhi
● Azitaka kulisaidia Shirika la Nyumba ili lijenge nyumba za gharama nafuu
● Asema Halmashauri zinunue nyumba zinazojengwa na NHC kwa ajili ya watumishi wao
● Alipongeza NHC kwa kasi ya ujenzi wa nyumba bora katika Halmashauriza Miji na Wilaya
● Azitaka kulisaidia Shirika la Nyumba ili lijenge nyumba za gharama nafuu
● Asema Halmashauri zinunue nyumba zinazojengwa na NHC kwa ajili ya watumishi wao
● Alipongeza NHC kwa kasi ya ujenzi wa nyumba bora katika Halmashauriza Miji na Wilaya
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba
na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline Sylvester Lubala Mabula
akisalimiana na Watumishi wa Hamashauri ya Mji wa Buchosa alipowasili
kusikiliza na kutatua migogoro ya ardhi
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba
na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline Sylvester Lubala Mabula
akipewa maelezo na mtaalam wa mifumo ya uwekaji kumbukumbu za umiliki wa
ardhi alipotembelea idara ya ardhi Wilayani Misungwi. Aliyoko katikati
ni Mkurugenzi wa Halmshauri hiyo Bw. Mshana.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba
na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline Sylvester Lubala Mabula na
Mbunge wa Chato Mhe.Dkt Medard Kalemani wakikagua eneo la Kijiji cha
Rusungwa lenye mgogoro mkubwa wa ardhi unaofanya wananchi wa kijiji
hicho kukosa ardhi ya kulima na uwekaji huduma za jamii kama shule baada
ya eneo la ekari 500 la kupewa mwekezaji.
Meneja wa NHC Mkoa wa Kagera
Bw. Deogratius Batakanwa akimpewa maelekezo na Naibu Waziri wa Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline Mabula ya kuhakikisha
kuwa anatoa elimu ya kutosha itakayowezesha wananchi, taasisi na
Halmashauri ya Muleba kukamilisha ununuzi wa nyumba zilizojengwa na NHC
Wilayani Muleba.Naibu Waziri alitembelea nyumba hizo na kulipongeza
Shirika la Nyumba kwa ujenzi wa nyumba bora.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba
na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline Sylvester Lubala Mabula
akiwa katika picha ya pamoja na Madiwani wa Halmashauri ya Muleba baada
ya kuhutubia Baraza lao na kuliomba liwezeshe ununuzi wa nyumba za
gharama nafuu zilizojengwa na NHC Wilayani humo. Pia aliagiza Baraza
hilo kushiriki kikamilifu katika kutatua migogoro mingi ya ardhi
iliyoko katika Wilaya hiyo.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba
na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline Sylvester Lubala Mabula
akikagua nyumba zilizojengwa na NHC eneo la Bombambili Mkoani Geita kwa
ajili ya kuuza. Amewataka wananchi na Halmashauri ya Mji wa Geita
kununua nyumba hizo ili kuliwezesha Shirika kuendelea kujenga nyumba
katika Halmashauri zingine.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline Sylvester Mabula akiwa na Mbunge
wa Chato Mhe. Dkt Medard Kalemani ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nishati
na Madini wakikagua nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na NHC Wilayani
Chato. Katika ziara hiyo Naibu Waziri ameishauri Halmashauri ya Chato
kununua nyumba hizo ili NHC iongeze ujenzi wa nyumba zingine kwa ajili
ya kukidhi mahitaji ya nyumba Wilayani humo.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba
na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline Sylvester Lubala Mabula
akisaini kitabu cha wageni katika Ofisi za NHC Mkoa wa Kagera
alipotembelea na kusalimiana na wafanyakazi wa Shirika hilo.
Meneja wa NHC Mkoa wa Mwanza
Injinia Benedict Kilimba akitoa maelezo ya mradi wa nyumba za gharama
nafuu zilizojengwa na NHC Bombambili Geita, kwa Naibu Waziri wa Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline Mabula alipotembelea
mradi huo. Mhe. Naibu Waziri ameziagiza Halmashauri nchini kusaidia
uwekaji wa miundombinu kwenye maeneo ya ujenzi wa nyumba hizo pamoja na
kutoa ardhi bure kwa NHC ili nyumba zinazojengwa ziwe na gharama nafuu
kwa mnunuzi.
Mkuu wa Wilaya ya Misungwi
Bibi Mwajuma Nyiruka akitoa taarifa ya sekta ya ardhi ya Wilaya yake
kwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt
Angeline Sylvester Lubala Mabula alipoitembelea Halmashauri ya Misungwi
kusikiliza na kutatua migogoro ya ardhi.
Baraza la Madiwani Muleba
wakimsikilza Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.
Dkt Angeline Mabula (hayuko pichani) alipohutubia Baraza hilo.
No comments:
Post a Comment