KUSHOTO NI MKUU WA WILAYA YA NJOMBE SARAH DUMBA,WA PILI KUTOKA KUSHOTI NI WAZIRI WA MAJI GERSON RWENGE NA WA MWISHO KUTOKA KUSHOTO NI MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA MJI WA NJOMBE EDWIN MWANZINGA WAKIWA KATIKA UKUMBI WA AGREEMENT NJOMBE MJINI KABLA YA SAFARI KUANZA YA KUTEMBELEA MIRADI
HAPA NI KABLA YA WAZIRI KWENDA KUTEMBELEA MIRADI YA MAJI NJOMBE
WAZIRI WA MAJI MHANDIS GERSON RWENGE AKIWEKA JIWE LA MSINGI KWENYE TENKI LA MAJI PELUHANDA LEO
MAJI YA CHANZO CHA MTO NYENGA NJOMBE MJINI
MKURUGENZI WA MAMLAKA YA MAJI NJOMBE MJINI DAUD MAJANI AKIONGOZA MSAFARA HUO BAADA YA KUFIKA KWENYE CHANZO CHA MTO NYENGA
Waziri Wa Maji Na Umwagiliaji Gerson Rwenge Ameahidi Kupeleka Gari Ili Kutatua Changamoto Ya Usafiri Inayoikabili Mamlaka Ya Maji Katika Halmashauri Ya Mji Wa Njombe Ambapo Ametaka Gari Hilo Likiletwa Litumike Kwa Malengo Yaliokusudiwa Na Si Vinginevyo.
Akizungumza Mara Baada Ya Kutembelea Miradi Ya Maji Iliyopo Katika Halmashauri Ya Mji Wa Njombe Waziri Rwenge Amesema Ili Kutekeleza Zoezi La Kusogeza Huduma Ya Maji Kwa Wananchi Wizara Itapeleka Gari Kwaajili Ya Mamlaka Ya Maji Na Kuhusu Chanzo Cha Maji Hagafiro Serikali Inakwenda Kuzungumza Na Serikali Ya India Ili Kutekeleza Mradi Huo.
Waziri Rwenge Amesema Mkoa Wa Njombe Unauhakika Wa Kupata Maji Kwa Asilimia 95 Ifikapo Mwaka 2020 Kwa Maeneo Ya Mijini Huku Vijijini Ikiwa Na Uhakika Wa Kufikisha Maji Kwa Asilimia 85 Ambapo Ameagiza Watumishi Wa Halmashauri Kutumia Kwa Malengo Yaliyokusudiwa Fedha Zinazoletwa Na Wizara Kwa Kuwalipa Wakandarasi.
Aidha Waziri Rwenge Akiweka Jiwe La Msingi Kwenye Tenki La Maji Peluhanda Amepongeza Kwa Jitihada Za Ujenzi Wa Tenki La Maji Ambalo Wananchi Kwa Kushirikiana Na Halmashauri Pamoja Na Wadau Wametekeleza Nakwamba Moyo Huo Wanapaswa Kuendelea Nao Ili Tatizo La Maji Liwe Historia Mjini Njombe.
Akisoma Taarifa Ya Mamlaka Ya Maji Njombe Mjini Mkurugenzi Wa Mamlaka Hiyo Daud Majani Amesema Mamlaka Inakabiliwa Na Changamoto Mbalimbali Ikiwemo Ukosefu Wa Gari Kwaajili Ya Uendeshaji Wa Shughuli Mbalimbali Za Mamlaka,Uchakavu Wa Miundombinu Ya Mabomba Na Kusababisha Maji Kupotea Na Kuchafuliwa Na Mabomba Yaliochakaa.
No comments:
Post a Comment