Waziri kuu, Kassim Majaliwa
akiteta na Askofu Mkuu wa Pili wa EAGT, Dkt. Brown Abel Mwakipesile
katika Ibada ya kumsimika Askofu huyo iliyofanyika kwenye kanisa la
EAGT Mlimwa West Mjini Dodoma Februari 7, 2016.
……………………………………………………………………………………………….
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema ataitisha kikao cha viongozi wa dini zote hivi kar
ibuni ili wapange na kuainisha ni mambo gani ambayo wanaweza kutoa ushauri kwa Serikali na kupata njia bora ya kuwahudumia Watanzania.
ibuni ili wapange na kuainisha ni mambo gani ambayo wanaweza kutoa ushauri kwa Serikali na kupata njia bora ya kuwahudumia Watanzania.
Ametoa ahadi hiyo leo mchana
(Jumapili, Februari 7, 2016) wakati akizungumza na mamia ya waumini
walioshiriki ibada ya kumsimika Askofu Mkuu wa Pili wa Kanisa la
Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT), Askofu Dk. Brown Abel
Mwakipesile iliyofanyika kwenye kanisa la EAGT la Mlimwa West nje kidogo
ya mji wa Dodoma.
Waziri Mkuu Majaliwa ambaye
alihudhuria ibada hiyo kwa niaba ya Rais Dk. John Pombe Magufuli
alisema: “Hivi karibuni nitaitisha kikao cha viongozi wa dini zote
kitakachojumuisha Maaskofu Wakuu, Masheikh na baadhi ya wachungaji ili
tukae na kubaini ni nini kifanyike ili kuisadia Serikali namna nzuri ya
kuboresha maisha ya Watanzania.”
Akijibu risala iliyosomwa na
Katibu Mkuu wa kanisa hilo, Dk. Leonard Mwizarubi, Waziri Mkuu alisema
Serikali imeanza kufanya mapitio ambayo yatawawezesha Watanzania kupata
huduma kwa urahisi.
“Katibu Mkuu pamoja na Baba
Askofu Mkuu wamegusia suala la upandaji wa gharama za vifaa vya ujenzi
pamoja na suala la makazi bora. Mwezi ujao tunaanza vikao vya Bunge vya
kupitia bajeti ya Serikali, tutaliangalia hili kwa kumshirikisha Waziri
wa Fedha… tutafanya mapitio katika hili ili mwananchi wa kawaida aweze
kumudu maisha,” alisema huku akishangiliwa na waumini hao.
Aliwaomba viongozi wa kanisa hilo
pamoja na waumini wake waendelee kuiombea nchi pamoja na viongozi wa
Serikali ya Awamu ya Tano kwani kazi ya kutumbua majipu waliyoianzisha
ina mitihani mikubwa.
“Kutokana na maombi yenu kwa
viongozi wakuu wa kitaifa nina imani Taifa hili litafika tunakotaka
liende. Endeleeni kutuombea kwa sababu kazi ya kutumbua majipu ina
mitihani mikubwa. Lakini pia napenda niwahakikishie kuwa Serikali hii
itatumbua majipu hayo kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu
zilizowekwa. Hakuna mtu ambaye ataonewa,” alisisitiza Waziri Mkuu.
Kuhusu mgogoro wa kiwanja cha
kanisa hilo kilichopo eneo la Ipagala, Waziri Mkuu aliahidi
kulishughulikia suala lao kesho asubuhi kabla hajaondoka kurejea Dar es
Salaam. “Kesho asubuhi nitamuita Mkurugenzi Mkuu wa CDA na kumtaka anipe
taarifa sahihi kuhusu mgogoro huu. Najua suala hili liko mahakamani,
lakini naamini Mkurugenzi anaweza kuwa kiungo kizuri kati ya wananchi
waliojenga eneo hili pamoja na kanisa ambao mnamiliki kiwanja husika”.
“Kama atapata eneo jingine na
kupima viwanja, kisha akawapatia hawa wananchi anaweza kuwa amesaidia
kuondoa mgogoro huu. Wananchi walienda mahakamani huku wakijua eneo lenu
limewekewa uzio, sasa wanagoma kutoka kwa sababu hawana mahali pa
kwenda,” aliongeza.
Mapema, akitoa hotuba yake,
Askofu Mkuu Dk. Mwakipesile alisema kanisa litaendelea kuiombea Serikali
ya awamu ya tano ili nchi idumu katika amani na utulivu.
Aligusia eneo la kanisa lililopo
kiwanja na 34, kitalu ‘E’, Ipagala East, Dodoma, ambalo ujenzi wa shule
yake umesimama kutokana na mgogoro baina yao na wananchi waliovamia eneo
lao kwa kujenga nyumba za kuishi licha ya kuwa eneo hilo
lilikwishawekewa uzio.
“Kama kanisa tumeshindwa
kukamilisha ujenzi wa shule kwa sababu wananchi hao walifungua kesi
mahakamani kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa. Tunaomba uamuzi wa kesi hii
uharakishwe,” alisema huku akishangiliwa.
Alisema kanisa hilo lina majengo
4,670 nchini kote na viwanja 420 ambavyo ni vya kujenga makanisa na
vituo vya kutoa huduma mbalimbali za kijamii.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa
kanisa hilo, Dk. Mwizarubi alisema katika risala yake kwamba wanaiomba
Serikali ifikirie kushusha bei ya vifaa vya ujenzi ili wananchi waweze
kuwa na nyumba bora za kuishi.
“Maisha bora maana yake ni kuwa
na nyumba bora. Tunaiomba Serikali yako ipunguze bei ya vifaa vya ujenzi
ili Watanzania waweze kuwa na makazi bora,” alisema huku akishangiliwa.
No comments:
Post a Comment