Waimbaji
wa nyimbo za injili, Stella Joel (kulia) ambaye ametunukiwa Tuzo ya
Heshima ya Shahada ya Uzamili ya Mahusiano na mwenzake Upendo Mbila
(kushoto), aliyetunukiwa Tuzo ya Heshima ya Shahada ya Uzamili ya
Uongozi wa Umma wakiteta jambo kwenye mahafali hayo ya pili ya Chuo cha
African Graduate University yaliyofanyika Dar es Salaam juzi.
Wahitimu wakiwa katika picha ya pamoja.
Paul Mbila (kulia), akimvika taji mama yake Upendo Mbila ambaye ni mwimbaji wa nyimbo za injili baada ya kutunukiwa tuzo Heshima ya Shahada ya Uzamili ya Uongozi wa Umma.
………………………………………………………………….
Na Dotto Mwaibale
Chuo
Kikuu cha African Graduate University kimewatunuku tuzo za heshima za
stashahada ya uzamili katika ngazi mbalimbali waimbaji wa nyimbo za
injili nchini kutokana na mchango wao katika jamii.
Akizungumza
wakati wa kukabidhi tuzo hizo kwa waimbaji hao katika mahafali ya pili
ya chuo hicho yaliyofanyika Dar es Salaam juzi Makamu Mkuu wa Chuo
hicho, Askofu Profesa Stephano Nzowa alisema ni jambo jema kuwakumbuka
watu mbalimbali waliolifanyia taifa mambo mazuri.
“Chuo
chetu kimeona ni vema kikawapa tuzo za heshima watu mbalimbali wakiwemo
wanamuziki wa nyimbo za injili kwani kupitia uimbaji wao wameweza kutoa
mafunzo kwa watu na wengine kuacha kutenda dhambi na kuamua kuokoka”
alisema Profesa Nzowa.
Baadhi
ya waimbaji wa nyimbo za injili waliotunukiwa tuzo hizo ni Rais wa
Shirikisho la Muziki Tanzania, Ado Novemba ambaye alitunukiwa tuzo ya
heshima ya udaktari, Stella Joel ambaye ametunukiwa Tuzo ya Heshima ya
Shahada ya Uzamili ya Mahusiano na Upendo Mbila aliyetunukiwa Tuzo ya
Heshima ya Shahada ya Uzamili ya Uongozi wa Umma.
Akizungumza
baada ya kupata tuzo hiyo Stella Joel alisema anamshukuru mungu kwa
kumuwezesha kupata tuzo hiyo na kuwa imemtia nguvu kuendelea kufanya
kazi ya mungu kupitia uimbaji.
Kwa
upande wake Upendo Mbila alitoa shukurani zake kwa chuo hicho kwa
kutambua mchango wa waimbaji wa nyimbo za injili kwa kuwapa tuzo hizo
ambazo ni muhimu kwao.
No comments:
Post a Comment