Baadhi
ya Vibanda vya Biashara vya Wafanyabiashara Ndogondogo Maarufu kama
Machinga Vikiteketea kwa Moto mara baada ya Wafanya Biashara hao wa Eneo
la Sido na Stendi ya Kabwe Jijini Mbeya kuanzisha Vurugu Baada ya
Kubomolewa Vibanda vyao vya Biashara katika maeneo waliyokuwa wakifanyia
Biashara Zao.
Jitihada
za kuzima Moto ulio washwa na Wamachinga wa Kabwe na Sido zikifanyika
kutoka kwa Jeshi la Zima Moto Jiji la Mbeya katika Vurugu zilizo Dumu
kwa Muda kuanzia Asubuhi ya Leo na kupelekea Wamachinga hao Kuchoma
Matairi Barabarani na Baadhi ya Masalia ya Vibanda vyao mara baada ya
Kubomolewa Vibanda vyao vya Biashara.
Jeshi la Polisi kikosi cha kutuliza Ghasia kikiwa Ngangari kuhakikisha hali ya Usalama ina kuwa Shwari na Vurugu kutoendelea...
Baadhi
ya wapiga Debe wa Stendi ya Kabwe wakiwa hawana nongwa na Mtu bali
wakiendelea kutimiza agizo la Rais Dkt.John Pombe Magufuli kufanya Usafi
kila Juma Mosi ya mwisho wa Mwezi na hapo wakiwa Sambamba na Vifaa vyao
vya kufanyia Usafi mbele ya Jeshi la Polisi kama waonekanavyo katika
Taswira.
PICHA ZOTE NA MR.PENGO MMG MBEYA.
No comments:
Post a Comment