Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Thursday, February 4, 2016

SHIRIKA LA TUNAJALI LA KABIDHI GARI KWA HALMASHAURI YA WILAYA YA WANGING'OMBE KWAAJILI YA SHUGHULI ZA AFYA


 GARI HILI LIMEKABIDHIWA NA MKUU WA MKOA KWA WILAYA YA WANGING'OMBE LILILOTOLEWA NA SHIRIKA LA TUNAJALI KWAAJILI YA SHUGHULI ZA AFYA.
 MENEJA  TUNAJALI FRANCISCO MELKIARD AKIONGEA MAELEZO KIDOGO KUHUSIANA NA KUPATIKANA KWA GARI HILO
 MENEJA TUNAJALI ANAMKABIDHI UFUNGUO WA GARI MKUU WA MKOA WA NJOMBE DKT REHEMA NCHIMBI
 HAPA AMEKWISHA KUKABIDHIWA  UFUNGUO WA GARI

 NA YEYE MKUU WA MKOA WA NJOMBE ANAMKABIDHI MUFUNGUO MKURUGENZI WILAYA YA WANGING'OMBE  MELKZEDECK HUMBE

 MKURUGENZI WILAYA YA WANGING'OMBE  MELKZEDECK HUMBE AKISHUKURU KWA MSAADA HUO



 PICHA YA PAMOJA NA MKUU WA MKOA BAADA YA KUKABIDHI GARI HILO

Halmashauri ya Wilaya ya Wanging'ombe Imepokea Msaada wa Gari Ambalo Litatumika Kwa Ajili ya Shughuli za Afya Katika Halmashauri Hiyo Ikiwemo Kukagua na Kuvitembelea Vituo Vinavyotoa Huduma za Afya Kwa Wananchi.

Akizungumza Wakati Akikabidhi Gari Hilo Lililotolewa na Shirika la Tunajali Mkoa wa Njombe, Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dkt. Rehema Nchimbi Amesema Gari Hilo Litasaidia Kutatua Changamoto ya Usafiri Kwa Watumishi wa Afya Iliyokuwa Ikiwakabili.

Aidha Dkt. Nchimbi Ameongeza Kuwa Licha ya Halmashauri Hiyo Kukabiliwa na Changamoto Mbalimbali Katika Sekta ya Afya Ikiwemo Dawa, Vitendanishi Pamoja na Vifaa Tiba , Amewataka Watumishi wa Afya wa Halmashauri Hiyo Wakiongozwa na Daktari wa Wilaya ya Wanging'iombe Wanalitunza Gari Hilo na Kulitumia Kwa Malengo Yaliyokusudiwa.

Dkt Nchimbi Amesema  Watumiaji Wanapaswa Kulitunza Kwa Umakini  Na Kuhakikisha  Watumishi Wa Afya Watunze Muda Wa Kwenda Kutatua  Kero  Mbalimbali Ambazo Zitakuwa Zinajitokeza Katika Zahanati ,Vituo Vya Afya Na Hospitali Pindi Watakapokuwa Wanapata Taarifa  Za Kutokea  Matatizo Ya Upungufu Wa Vitendanishi Na Vifaa Tiba Katika Wilaya Hiyo.

Awali Akizungumzia Hatua ya Shirika la Tunajali Kutoa Gari Hilo, Meneja wa Shirika Hilo Mkoa wa Njombe Francisco Melkiard Amesema ni Mwendelezo wa Tunajali Katika Kusaidia Kutatua Changamoto Zinazoikabili Sekta ya Afya Kwa Halmashauri za Mkoa wa Njombe.

Kwa Upande Wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Wanging'ombe Melkzedeck  Humbe Amelishukuru Shirika Hilo , na Kuahidi Kuwa Watalitunza na Kulitumia Gari Hilo Kwa Malengo Yaliyokusudiwa Huku Akiwaomba Wadau Wengine wa Afya Kuendelea Kusaidia Kutatua Changamoto Zinazoikabili Sekta ya Afya.

No comments:

Post a Comment