Waziri wa nchi ofisi ya
rais TAMISEMI, utumishi na utawala bora, George Simbachawene wa kwanza
kushoto akiwaambia jambo mkuu wa mkoa wa Pwani mhandisi Evarist Ndikilo
wa katikati na wa kulia mganga mkuu hospital ya Rufaa ya Tumbi dk. Peter
Datan wakati alipotembelea shirika la elimu Kibaha juzi. (Picha na
Mwamvua Mwinyi)
…………………………………………………………………………………………………………………………..
Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha
Waziri wa nchi ofisi ya
rais TAMISEMI, utumishi na utawala bora, George Simbachawene amesema
ataunda tume ya watu wachache kutoka wizara hiyo haraka iwezekanavyo ili
kuchunguza idara na vitengo vyote katika shirika la elimu Kibaha (KEC)
ndani ya wiki mbili.
Amesema amefikia hatua
hiyo baada ya kubaini tatizo kubwa la uongozi hivyo ipo haja ya
kuchunguza hali iliyopo kuanzia juu hadi chini.
Aidha Simbachawene
alisema tume hiyo itakuwa na kazi ya kupita kila idara na kitengo
kuchunguza mambo atakayoyaelekeza kwa siku 14 kisha mwezi march mwaka
huu atarejea kufanya ziara na kuzungumza na watumishi.
Alielezea kuwa kuna
kila sababu ya kutafakari muundo mzima wa shirika na kuweka mikakati,
sheria na mipango ya kisasa na kuondokana na ile iliyopitwa na wakati.
Aliyasema hayo juzi
katika ziara yake ya kikazi ya siku moja aliyoifanya shirika la elimu
Kibaha ambapo alipata fursa ya kutembelea maeneo ya uwekezaji na shirika
kijumla.
Simbachawene alisema
katika shirika hilo kuna wachache wanaonufaika na kuneemeka kwa kula
hadi wamevimbilwa huku wengine wakiwa wanadidimizwa kimaslahi na kukosa
haki zao za msingi.
Alimtaka mwenyekiti wa
bodi mpya ya shirika hilo Patrick Makungu na viongozi wengine katika
bodi hiyo, kuwa na mawazo mapya ya kuendesha shirika badala ya kufanya
kazi kwa mazoea ili kurudisha maendeleo yaliyokuwepo miaka ya nyuma.
Alisema shirika la
elimu Kibaha lina miradi mingi, ardhi kubwa na uwekezaji mkubwa hivyo
waitumie kujiongezea kipato kwa maslahi ya Taifa na vizazi vijavyo.
Simbachawene alieleza KEC inayumba na kuondoa taswira ya maendeleo na uchumi wake wakati ina vitega uchumi na ardhi kubwa.
“Serikali ya awamu ya
tano chini ya rais Magufuli ipo kwa ajili ya kuinua uchumi wa nchi na
haitokuwa tayari kuona mashirika ya aina hii yanashushwa hadhi yake na
watu wachache na kuwanyima haki watumishi uhuru wa kutembea kiajira na
haki zao za msingi “
” Ipo haja ya
kuchunguzana na kufanya maamuzi makini kwa kufuata misingi, sheria,
kanuni na haki za kiutumishi”alisema Simbachawene.
Hata hivyo alisema
uwekezaji wa kampuni ya organia kutoka Egypt iliyowekeza kwenye shirika
hilo ni mzuri na wenye tija lakini unaonekana haukuata taratibu na
kusababisha maswali kutoka kwa watumishi.
Awali mkurugenzi wa
shirika la elimu Kibaha Dk. cyprian Mpemba alisema shirika linakabiliwa
na changamoto mbalimbali ikiwemo kupokea wagonjwa wengi 400 hadi 450 kwa
siku na madawa.
Dk. Mpemba alitaka
serikali kufikisha fedha kwa wakati kwani ni muda mrefu sasa fedha
wanazoahidiwa wanatumiwa pungufu tofauti na kiwango wanachoomba hivyo
kushindwa kukidhi mahitaji.
Nae mganga mkuu wa
hospital ya Rufaa ya Tumbi, dk. Peter Datan alisema kitengo cha maafa
hususan ajali (Trauma center) kinakabiliwa na ukosefu wa fedha kwa zaidi
ya miaka mitatu sasa.
Katika hatua nyingine
waziri huyo alipokea kero mbalimbali kutoka kwa watumishi wa shirika
hilo ikiwa ni sanjali na wastaafu shirikani hapo kukosa stahiki zao.
Kero nyingine ni
kuondolewa mradi wa kuku ulikuwa ukiingiza bil. 1 na kuingizwa mradi wa
mkataba wa Organia ambao hawauelewi maslahi yake, upungufu wa nyuzi,
madawa, fedha za allowance na walimu kutopandishwa madaraja kwa miaka
sita sasa.
Simbachawene alipokea
kero hizo na kuahidi kuzifanyia kazi ambapo kwa upande mwingine aliitaka
mganga mkuu dk. Datan kukumbushia fedha walizoahidiwa serikalini ili
ombi lao lishughulikiwe haraka.
No comments:
Post a Comment