Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe, Ummy Mwalimu
akitoa shukurani za dhati kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli mbele ya Mufti Mkuu wa Tanzania pamoja
na baadhi ya Viongozi waliohudhuria mkutano wakati siku ya kuruhusiwa
kurejea nyumbani kwa Mufti huyo, leo Jijini Dar es Salaam.
Mufti
Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeiry Bin Ally (Kushoto) akitoa
shukurani za mbele ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee
na Watoto, Mhe, Ummy Mwalimu pamoja na baadhi ya Viongozi waliohudhuria
mkutano wakati siku ya kuruhusiwa kurejea nyumbani kwa Mufti huyo, leo
Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu
Tanzania (BAKWATA), Sheikh Suleiman Lolila.
Katibu
Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), Sheikh Suleiman
Lolila akisoma taarifa ya shukurani toka kwa Mufti Mkuu wa Tanzania
Sheikh Abubakary Zubeiry Bin Ally mara baada ya kupata matibabu na
kuruhusiwa kurejea nyumbani toka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili-Taasisi
ya Moyo ya Jakaya Kikwete leo Jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya Viongozi wa Serikali, Viongozi wa Vyama vya Siasa, Viongozi wa
Taasisi mbalimbali, Masheikh, Madaktari pamoja na Waandishi wa Habari
waliohudhuria mkutano Hospitalini hapo wakifuatilia taarifa toka kwa
Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeiry Bin Ally (hayupo
pichani) leo katika Ukumbi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete iliyopo
Jijini Dar es Salaam.(Picha zote na Benedict Liwenga)
Mufti Mkuu wa Tanzania asifia huduma bora za Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Na Benedict Liwenga-Maelezo.
MUFTI
Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeiry Bin Ally amepongeza huduma
bora alizopatiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Kitengo cha
Taasisi ya Moyo cha Jakaya Mrisho Kikwete mara bada ya kupata ruhusa ya
kurejea nyumbani.
Pongezi
hizo amezitoa leo Jijini Dar es Salaam mbele ya Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu pamoja na
Viongozi wengine wa Serikali, Viongozi wa Vyama vya Siasa, Viongozi wa
Taasisi mbalimbali, Masheikh, Madaktari pamoja na Waandishi wa Habari
waliohudhuria mkutano Hospitalini hapo.
Mufti
Zubeiry ameeleza kuwa, yeye pamoja na Familia yake pamoja na Baraza la
Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) wanatoa shukurani za dhati kwa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Joseph Magufuli kwa
msaada wa kumwezesha kupata matibabu hospitalini hapo pamoja na watu
wengine waliofanikisha matibabu hayo kwa namna moja au nyingine.
Amesema
kuwa Hospitali hiyo ina Mabingwa wazuri waliobobea wenye uwezo na
endapo wakitumika vizuri hali ya huduma ya afya hospitalini hapo
itavutia kama zile zilizoko nje ya nchi, pia ameiomba Serikali kuona
umuhimu wa kuangalia suala la Madakati, vitendea kazi, pamoja na Wauguzi
hospitalini hapo ili huduma bora zizidi kutolewa.‘’Namuomba Rais wetu
kuitazama Hospitali hii chini ya Wizara ya Afya pamoja na mabingwa wetu
tulionao kwani hapa ni gereji ya binadamu hivyo panapaswa kuangaliwa kwa
makini’’, alisema Mufti Zubeiry.
Katika
hatua nyimngine, Mufti Zubeiry amewashukuru Marais Wastaafu wa Serikali
ya Tanzania akiwemo Mhe. Benjamin William Mkapa pamoja na Mhe. Jakaya
Mrisho Kikwete kwa kufika kumfariji kipindi yuko mgonjwa.‘’Pia
ninawashukuru Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa na
familia yake, Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu, Mwanasheria Mkuu wa
Serikali pamoja na Naibu Spika Turia Ackson kwa moyo wao wa kuja
kunifariji’’, alisema Mufti.
Kwa upande
wake Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe.
Ummy Mwalimu ameeleza kuwa, kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe, John Pombe Joseph Magufuli amezipokea shukurani hizo toka
kwa Mufti Mkuu wa Tanzania kwa kupona na kuruhusiwa hospitalini hapo na
pia amewashukuru Madaktari bingwa na Wauguzi wote walioshiriki katika
kumtibu Mufti huyo.
‘’Mmetupa
changamoto sisi ya kutaka kufanya vizuri zaidi, ni matarajio yetu sisi
kama Serikali kuona viongozi wote wa Tanzania akiwemo Mufti Mkuu na
wengine wanatibiwa katika Hospitali yetu ya Taifa ya Muhimbili, hivyo
mmetusaidia sana kutuma ujumbe kwa Watanzania kuwa tunaweza kutumia
hospitali zetu katika kuwatibu viongozi wetu nchini’’, alisema Mhe.
Ummy.
Almeongeza
kuwa, Wizara ya Afya itaendelea kujitahidi kuboresha huduma za afya
hospitalini hapo, ikiwemo suala la Wataalamu, vifaa vya tiba pamoja na
kuongeza hamasa kwa Watanzania ya kutibiwa hospitalini hapo kwakuwa
Mufti pamoja na baadhi ya na viongozi wengine ambao wamewahi kutibiwa
hospitalini hapo wameonyesha moyo wa kuboresha zaidi huduma hospitalini
hapo.
No comments:
Post a Comment